Tumezoea mara nyingi Apple ndio wamekuwa wakilalamika kuibiwa ubunifu wa simu zao lakini sasa ni wao ndio wamepatikana na hatia nchini China kwa kosa la kuiga ubunifu wa muonekano.
Kitengo cha haki miliki za ubunifu na mawazo ya kibiashara cha nchini China kimeikuta Apple na hatia ya kuiga ubunifu kutoka kampuni ndogo ya utengenezaji simu ya nchini humo.
Kampuni hiyo inafahamika kama Shenzhen Baili na simu za iPhone 6 zimekutwa na hatia ya kuiga muoneakno wa simu ya 100C kutoka kampuni hiyo ya China.
Katika hukumu hiyo inasemekana muonekano wa iPhone 6 na 6 Plus unafanana sana na simu ya 100C kiasi cha kumfanya mnunuaji kuwa vigumu kutambua tofauti kati ya iPhone 6 na simu hiyo kwa haraka haraka.
Soko la China ni moja la soko muhimu sana kwa sasa kwa ukuaji wa simu zake za iPhone, data zinaonesha zaidi ya asilimia 25 ya mauzo yake kwa sasa yanatoka nchini humo na hivyo inategemewa maaumizi haya yanaweza athiri mapato kwa kampuni hiyo maarufu duniani.
Kampuni ya Apple imefungua kesi ya rufaa kupinga matokeo hayo ya kesi. Kwa sasa wataweza endelea kuuza simu hizo, ila kama wakishindwa katika kesi yao ya rufaa basi itakuwa marufuku kwa simu hizo kuuzwa nchini China.
Vipi kwa mtazamo wako, je unadhani ni kweli simu ya iPhone 6 na 6 Plus zina muonekano wa karibu sana na simu ya 100C iliyotengenezwa na Shenzhen Baili?
Vyanzo: Forbes na mitandao mbalimbali