Kampuni ya TTCL imeingia mkataba na kampuni ya Avanti Communications Group ya Uingereza ili kampuni hiyo iweze kusaidia kuiwezesha huduma yake ya intaneti ya kasi (broadband) kuweza kuwafikia ata wale walio nje ya maeneo yaliyofikiwa na mkongo wa intaneti wa taifa (Fibre).
‘Kupitia teknolojia ya ‘Ka-band satellite’ ya Avanti tunategemea itatoa huduma ya intaneti ya kasi ya broadband kwa wateja wetu nchi nzima ambao wanategemea kupata huduma ya kiwango cha juu kabisa’ – Kamuhisha Kazaura, TTCL
Kupitia teknolojia ya satelaiti inayomilikiwa na kampuni ya Avanti, TTCL itaweza kutoa huduma za intaneti kwa wateja wake walio nje ya uwezo wa kufikiwa na huduma ya intaneti kupitia waya (mkongo). Satelaiti ya kampuni hiyo inaweza kurusha signo zake Tanzania nzima, hivyo kwa maofisi ya serikali na yasiyo ya kiserikali yaliyo ndani ndani mbali kabisa na mkongo wa taifa wataweza kupata huduma ya intaneti kwa urahisi zaidi kupitia kuwekwa kwa vifaa vya kupokea signo hizo za intaneti zinazorushwa kupitia huduma ya satelaiti ya Avanti.
No Comment! Be the first one.