Programu endeshaji (OS) ya Windows 10 itaanza kupatikana ifikapo tarehe 29 mwezi wa saba. Na zaidi ya hapo kama wewe ni mtumiaji wa Windows 7 au Windows 8 zilizopatikana kihalali basi tegemea kuweza kufanya sasisho (update/upgrade) bure kabisa kwenda Windows 10. Ila kwa wale ambao wanatumia matoleo ya kiwizi ya Windows 7 na 8 basi hawataweza kusasisha bure, itawabidi walipe ndio wataweza kufanya hivyo.
Kama unatumia matoleo ya Windows 7 Starter, Windows 7 Home Basic, Windows 7 Home Premium, Windows 8, au Windows 8.1 utaweza kusasisha kupitia intaneti kwenda toleo la Windows 10 Home bure kabisa. Na kwa watumiaji wa Windows 7 Professional, Windows 7 Ultimate, Windows 8 Pro, au Windows 8.1 Pro wataweza nao kusasisha kompyuta zao kwenda Windows 10 Pro bure. Na ofa hii itakuwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja kuanzia tarehe 29 mwezi wa saba mwaka huu.
Inakuwaje kama unatumia nakala za wizi?
Kama unatumia Windows 7 au 8 za wizi, au pia kama unataka kununua DVD ya Windows 10 basi itakugharimu takribani tsh 238,000/= (Dola 119 za Kimarekani) kwa toleo la Windows 10 Home, na kwa wale wanaotaka toleo la Windows 10 Pro basi itawabidi watumie takribani tsh 400,000/= (Dola 199 za Kimarekani).
Je unafahamu kipya kwenye Windows 10? Bofya HAPA kufahamu zaidi!
[socialpoll id=”2274730″]
Asante na endelea kutembelea mtandao wako wa TeknoKona!
No Comment! Be the first one.