Hawlett-Packard (HP) ambayo ni kampuni Nguli kwenye masuala ya kompyuta na vifaa vya uchapishaji inategemewa kupitia mabadiliko makubwa. HP iliundwa takribani miaka 75 iliyopita huko Palo Alto, California na ndipo makao makuu hadi sasa. HP imeweza endelea licha ya kuwa ikipata michuano mikali na kampuni zingine kama Oracle na IBM, kuanzia mwaka 2012 chini ya uongozi wa Bi. Meg Whitman imeweza kujisogeza mbele zaidi katika teknolojia/biashara ya kompyuta na mashine za uchapishaji (printa).
“Wazo letu la kutenga Hp katika makampuni mawili yanayoongoza sokoni linasisitiza maazimio yetu na pia linaendana na plani zetu” alisema Whitman
Siku ya jumatatu kampuni imetengaza plani zake za kutenganisha biashara ya kompyuta na biashara ya printa na kuleta kampuni mbili tofauti; Hawlett-Packard Enterprise (HP Enterprise) itakayojikita katika biashara kubwa za kiteknolojia kama kwenye masuala ya data za ‘Cloud’, na vifaa vingine kwa ajili ya maitaji ya data kubwa za kiofisi na HP Inc itakayokuwa inajihusisha na biashara za kompyuta, printa na vifaa vingine kwa ajili ya watumiaji wa kawaida. Licha ya biashara hizo mbili kuwa zinafanya vizuri tuu kampuni inaamini zitafanya vizuri zaidi endapo zikitenganishwa.
Biashara ya kompyuta na printa itatumia jina la ‘Hp Inc’ itaendeshwa na aliyekuwa mkuu wa kitengo cha kompyuta na printa, Bwana Dion Weisler na cheo chake atakuwa CEO, wakati Bibi Meg Whitman ambaye ndio alikuwa Mkurugenzi Mkuu (CEO) kwa sasa, yeye atakuwa CEO wa kitengo cha Hawlett-Packard Enterprise (HP Enterprise). Bw, Pat Russo ndio atakua mwenyekiti wa pande hizo mbili.
Kugawanyika huku kulikua katika majadiliano zaidi ya mwaka, kampuni imeamua kutilia mkazo kuwaridhisha wawekezaji wake na pia kufikisha malengo iliyojiwekea kiufahisi. Kampuni mama itatoa uhuru, mali ghafi, na muono kwa kila kampuni. Kimapato kampuni hiyo imekuwa ikifanya vizuri. HP ilikuwa namba moja katika uuzaji wa kompyuta kwa miaka mingi lakini walipokonywa nafasi hiyo na Lenovo, kwa sasa HP inashika nafasi ya pili, ila kwenye biashara ya printa bado HP hana mshindani.
No Comment! Be the first one.