Ni wazi kuwa wengi wetu huwa tunatumia simu zetu kutwa nzima. Na wengine usiku kucha – saa nyingine tunapitiwa na usingizi wakati tunazitumia – kioo cha simu janja ni rahisi kupata uchafu
Kuna wengine kama mtu mweupe asingegundua ‘Screen Protector’ sijui simu zetu zingekuwa na kioo cha hali gani hivi sasa
Kuna wengine wakiona simu zao zina vumbi kidogo tuu katika sehemu ya kioo, hao mbio mbio kufuta na nguo walizo nazo. Hii ni mbaya kwani kuna nguo spesho ambazo zinatakiwa kufuta kioo hicho
NJIA
> Tumia nguo (kitambaa) laini kabisa kile kilichotengenezwa kwa kutumia pamba 100% katika kufuta uchafu uchafu. Nguo ambazo sio za pamba na zina shuruba kama taulo hazifai kutumia maana zinaweza zikaharibu kioo cha simu janja yako
> Kwa sehemu zenye uchafu sugu, futa kioo kwa kutumia nguo laini sana (pamba) ambayo itakua imeangushiwa tone la maji. Kamwe usimimine maji moja kwa moja kwenye kioo cha simu. Na kingine cha muhimu hakikisha kuwa simu yako haipo kwenye chanzo chochote cha umeme kama vile ‘power bank’ au umeme wa ukutani
> Kamwe usitumie Amonia, dawa za kusafisha madirisha au hata sprei ya aina yeyote. Unyevu nyevu unaweza ukaingia katika sehemu za wazi na kuweza kuharibu simu janja yako (Pia kumbuka kuwa hakuna Warantii kwa kifaa kilichoharibiwa kwa kimiminika kama vile maji)
> Ukiwa katika usafishaji wa kioo cha simu yako, pia ni vyema kusafisha kitufe cha nyumbani. Futa kitufe hicho pole pole na kwa uangalifu kwa kutumia kitambaa kilaini kabisa au pamba. Ukifanya usafi huo kwenye simu kama za iPhone (kuanzia 5s na kuendelea) itasaidia Touch ID iweze fanya kazi vizuri
Pia epuka kuweka maji mengi kwenye nguo laini ambayo utaitumia katika kusafisha kioo cha simu janja yako. Mpaka hapo kifaa chako kitakua safi kabisa.
Soma Pia: Jinsi Ya Kusafisha Kioo Cha Laptop Au TV
One Comment
Comments are closed.