fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Apple IPhone simu Smartphones

Apple Waacha Kutengeneza Tena iPhone 12 Mini!

Apple Waacha Kutengeneza Tena iPhone 12 Mini!

Spread the love

Kwa wale amabao wanapenda simu janja za iPhone ambazo ni ndogo na zinakaa vizuri katika mikono yao matoleo haya (kama iPhone 12 Mini) yalikua ndio kimbilio lao.

Unaweza ukajiuliza ni kwanini hili limetokea mpaka kampuni iwe na uamuzi wa kutoendelea na uzalishaji wa simu hii, lakini kikubwa ni kwamba mauzo ya toleo la aina hii ya simu yamekua ni madogo sana.

SOMA PIA  Apple na Oprah kufanya kazi kwa pamoja

Ukiachana na hilo ni kwamba bado kampuni inakuja na toleo la iphone 13 ndogo ambayo inaweza ikajulikana  kama iPhone 13 Mini  ndani ya mwaka huu.

Vioo Vya Matoleo Ya iPhone Ndogo

Vioo Vya Matoleo Ya iPhone Ndogo

Vyanzo mbali mbali vimesema kuwa pengine toleo hilo halikuafanya vizuri sokoni kwani Apple walitoa toleo la pili ya iPhone SE (ambayo nayo ni ndogo) miezi sita baada ya kutoa tolea la iPhone 12 Mini.

SOMA PIA  Tarehe ya uzinduzi wa simu janja OnePlus Nord 2 5G yafahamika!

Inakuwa ni vigumu kwa yeyote ambae anapenda iPhone ndogo kuhama kutoka iPhone SE (toleo la pili) na kwenda kununua iPhone 12 mini ndani ya kipindi cha miezi sita tuu.

iPhone 12 ikiwa na iPhone 12 Mini

iPhone 12 ikiwa na iPhone 12 Mini

Aidha vyanzo mbalimbali bado vinadai kwamba Apple wataacha kabisa kutengeneza simu zenye vioo vidogo vya inchi 5.4 ifikapo mwaka 2022.

SOMA PIA  BlackBerry Venice: Picha za Simu ya Android Kutoka BlackBerry Zavuja

CHANZO

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, wewe unaona ni sawa kwa kampuni kuacha kuzalisha toleo hilo?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania