fbpx

Oppo Reno 10X Zoom: Hili ndio toleo rasmi kwa mashabiki wa FC Barcelona

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kama wewe ni shabiki kindakindaki wa timu ya FC Barcelona ya nchini Uhispania, Oppo Reno 10X Zoom FC Barcelona Edition inaweza ikawa simu nzuri kwa ajili yako.

Oppo, kampuni ya utengenezaji simu ya nchini Uchina imetengeneza simu ambayo ni maalumu kwa mashabiki wa timu hiyo ya FC Barcelona.

Muonekano wake nje na ndani umepambwa kwa rangi zinazotumiwa na timu hiyo  Nyekundu na Buluu kuonesha uhalisia wa Barca ambao ni mabingwa wa La Liga.

Oppo Reno 10X Zoom FC Barcelona Edition

Oppo Reno 10X Zoom FC Barcelona Edition

Baadhi ya sifa za simu hiyo unaweza kuangalia hapo chini.

INAYOHUSIANA  Simu rununu Realme 2 Pro imetoka

Oppo Reno 10X Zoom FC Barcelona Edition.

Prosesa  Qualcomm SDM855 Snapdragon 855
Network  GSM / CDMA / HSPA / EVDO / LTE
Ukubwa wa Kioo  6.6 inches (1080×2340) (AMOLED)
Mfumo endeshi OS  Android 9.0 (Pie)
Ukubwa wa uhifadhi  128GB, 8GB RAM
Kamera ya Nyuma  48-megapixel (f/1.7) + 13-megapixel (f/3.0) + 8-megapixel (f/2.2)
Kamera ya Selfie 16-megapixel (f/2.0)
ujazo wa Betri  Li-Po 4065 mAh (Haichomoki)

oppo

Kampuni ya Oppo ambayo ni sehemu ya wadhamini wa timu ya FC Barcelona imeanza kuuza simu hiyo mwishoni mwa mwezi Julai katika nchi ya China, Spain, India, Holand, France na baadhi ya nchi za Ulaya.

INAYOHUSIANA  Kuingia sokoni kwa BlackBerry Evolve

Soma uchambuzi wa simu nyingine mbalimbali -> Teknokona/Uchambuzi

Wale wapenzi wa Barca unaweza kuipata simu hiyo kwa bei ya TShs 2,040,000/-

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.