Vita baridi kati ya Marekani na Uturuki inaendelea kwa mataifa yote mawili kujibu mapigo baada ya rais Trump kuweka vikwazo kwa serikali ya Uturuki na wananchi wake kwa ujumla.
Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdoğan amewataka wananchi wake kuzisusia bidhaa za Marekani zikiwamo simu aina ya iPhone huku pia akiwataka kubadili fedha zao za kigeni, vito vyao vya thamani kama dhahabu kuwa pesa ya Uturuki.

Akizungumzia kuhusu kususia au kwa lugha nyingine kutonunua iPhone. Rais huyo aliwataka wananchi wake ambao idadi yao ni milioni 80, kuchangamkia simu za Samsung badala ya iPhone, na kwamba watafanya vizuri zaidi kununua simu zinazotengenezwa nchini mwao aina ya Venus.