fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Mtandao wa Kijamii TikTok

TikTok Kuja Na Video Ndefu Kwa Wote!

TikTok Kuja Na Video Ndefu Kwa Wote!

Spread the love

Ni wazi kwamba kipengele cha kurekodi video ndefu katika App ya TikTok kimekua katika majaribu tangi mwezi disemba mwaka 2021.

Kumbuka kwa sasa video ambazo zimezoeleka sana katika App hiyo ni zile za dakika moja. Kutoka dakika moja mpaka dakika tatu ndio utakua umbali wa mwisho kabisa.

app ya tiktok

TikTok

TikTok wanafanya hivi makusudi ili kuwezesha wabunifu kuwa na uwanja mkubwa katika ubunifu wao wakati wanaanda video. Kwa kifupi ni kwamba kikwazo cha muda kimepunguzwa.

Unaweza ukawa unajiuliza kwamba mbona hata hapo awali ulikua unaona video ndefu tuu, na hii isiwe ni habari tena kwako. Kwa zamani ni kwamba walichaguliwa wabunifu wachache tuu ambao walikua wanaweza tengeneza video vya urefu mkubwa.

Kwa sasa mtandao unaachia kipengele hichi kwa watumiaji wote wa TikTok na toleo litaanza patikana siku za usoni  kama bado halijaanza patikana.

Muoenkano Wa Ndani Wa TikTok (Mfano)

Muoenkano Wa Ndani Wa TikTok (Mfano)

Kingine cha kufikiria hapa ni kwamba je video ndefu zikiwa nyingi zitaathiri App ya TikTok kwa aina moja au nyingine? kumbuka App yenyewe ina kasumba ya kuwa inakula sana MBs

SOMA PIA  Ujumbe wa kejeli umekuwa msukumo mkubwa mtu kufanyiwa upasuaji

Pata picha video zikiwa ndefu ndefu tuu? kwangu nadhani hata matumizi (watu kutumia App mara kwa mara) yatapungua sana.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment hili umelipokeaje? na unadhani lina tija gani?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania