Kampuni ya Apple wameamua kutunisha misuli yake kwa kuvamia Teknolojia inayokua kwa kasi zaidi ya ‘Virtual Reality’ (VR) inayomwezesha mtumiaji kuweza kutazama picha za video kutoka nyuzi 360 za video hizo.
Apple imemwajiri mtaalamu mkubwa wa masuala ya VR, Doug Bowman ambaye amekua akifanya tafiti zilizofanikiwa sana katika miundo ya VR na 3D.
Kuajiriwa kuwa Bowman, kumetafsiriwa kuwa Apple hawana dhamira ya kuacha teknolojia ya VR ipite ivi ivi. Baadhi ya mitandao maarufu duniani kama MacRumours, imesema si jambo la kushangaza Apple kuamua kujikita kwenye teknolojia hiyo inayokua kwa nguvu.
Baadhi ya makampuni makubwa ya mambo ya teknolojia kama Microsoft, Google na Sony tayari wameanza kujikita katika teknolojia hii kwa kiasi kikubwa, sasa ushindai unaongezeka maradufu.
Awali, ilikuwa kama tetesi kuwa Apple huenda wakaja na techolojia iliyopachikwa jina la iVR kama ilivyo kwa iPhone, iMac, iPad n.k., lakini huenda apple wakaiita teknolojia hii Apple Virtual Reality kama sehemu ya upya wa mpango huu.
Bowman hatakuwa mtu wa kwanza kujiunga na Apple kuhusiana na VR. Mwanzoni mwa mwezi huu Apple imewaajiri wataalamu mbalimbali ambao watakuwa kwenye kikosi kitakachoongozwa na Bowman ili kufanikisha zoezi hili. Tayari wataalam wa ‘Face-Tracking, Emotion-Reading, wamepata ‘shavu’ linalotafsiriwa kuwa hatua za kufikia AVR.
Apple wameshindwa kusema lolote kuhusu kuajiriwa kwa Bowman, lakini Akauti ya Bowman ya Linked-In ilifutwa punde tu baada ya tetesi za kuajiriwa kuzagaa.
Makala inayochambua teknolojia hii ya ‘Virtual reality’ ilishaelezewa kipindi cha nyuma katika mtandao huu. Unaweza kuisoma tena kwa kubonyeza Hapa.
Chanzo cha habari hii ni Mtandao wa Mashable na MacRumours.
No Comment! Be the first one.