Mtandao ambao unafanana na Twitter wa Weibo wa nchini China umetangaza kwamba utawaruhusu watumiaji wake kuandika posts zinazozidi herufi 140 kuanzia tarehe 28 mwezi wa kwanza.
Ingawa ki ukweli ni kwamba kwa kuanzia posts zitaonesha herufi 140 za kwanza na kutakuwa na link ambayo itampeleka mtumiaji katika ujumbe wote.
Mtandao wa Twitter ambao bado unazuia watumiaji wake kuandika posts tweets zinazozidi herufi 140 sasa utakua katika shinikizo la kuondoa kizuizi hicho kutokana na ukweli kwamba mjadala juu ya idadi za herufi mtu anaweza kutumia katika mtandao huu imekuwa mingi.
Mtandao huo wa china Weibo umesema kwamba kwa watumiaji mahususi wa mtandao huu ndio watakao weza kuona post zao (zilizozidi herufi 140) zote bila ya kufungua link lakini kwa watumiaji wengine hawataweza kufurahia uhuru huu mpaka baadae kidogo.
Tetesi za Twitter kuongeza idadi ya herufi ilipokewa kwa hisia tofauti tofauti katika mtandao huo ambao ulianzishwa mwaka 2006 mwezi Machi na watu watatu Jack Dorsey, Evan Williams, Biz Stone, na Noah Glass. Hadi mwaka 2012 kulikuwa na watumiaji milioni 100 ambao wanatuma walau tweets milioni 340 kila siku, mtandao huu ni mmoja kati ya mitandao iliyotembelewa zaidi kwa mwaka 2015.
Soma zaidi kuhusu tetesi za Twitter kuruhusu herufi zaidi ya 140 HAPA
Weibo ni mtandao ulioanzishwa huko China na unafanana na mtandao wa Twitter, ni mtandao maarufu huko Uchina ulianzishwa mnamo mwaka 2009 baada ya mitandao kama Twitter kufungiwa katika nchi hiyo ambayo inasheria kali za mitandao.
No Comment! Be the first one.