Njia mpya imepatikana ambayo inatengeneza almasi zinazofanana na zile ambazo huchimbwa ardhini, hatua hii ya kiteknolojia inategemewa kupunguza utegemezi wa almasi kutoka ardhini hivyo kupunguza migogoro ya kisiasa na uharibifu wa mazingira.
Almasi kwa asili inapatikana kutokana na mgandamizo mkubwa na joto kubwa takribani kilomita 140 hadi 190 ndani ya ardhi, uundaji wa madini haya huchukua kati ya miaka bilion 1 hadi bilioni 3 (hii ni karibu asilimia 25 hadi 75 ya umri wa sayari yetu ya dunia). Madini haya ni adimu sana duniani hivyo sokoni ni ghari na pia yamesababisha migogoro mingi ya kisiasa katika nchi mbalimbali hasa Africa ya kati na magharibi baada ya watu kuanza kugombea migodi ya madini haya ghari na adimu.
Zipo njia tatu za kutengeneza almasi viwandani, Moja Joto kali na mgandamizo mkubwa (High Temperature High Pressure) hapa almasi hutengenezwa kwa kutumia joto kali na mgandamizo mkubwa katika kaboni. njia ya pili ni ya kutuamisha mvuke wa kemikali (Chemical Vapour Deposition) njii hii unahitaji almasi ya kuchimba ndogo kama ukucha kisha kwa kuutuamisha mvuke wenye kemikali za kaboni na haidrojeni basi hufanya almasi iote katika kile kipande kidogo cha asili. Njia ya tatu ni kwa kutumia ultrasound ila hii bado hijaanza kutumika kutengeneza almasi kibiashara.
Almasi hii ya kutengenezwa itakuwa na bei ndogo kwa karibu asilimia 50 ukilinganisha na almasi ya kuchimbwa, kwa mwaka 2013 tani zipatazo 1500 za almasi zilitumika katika shughuri za viwandani na 90% ya hii almasi ilikua ni ile ya kutengeneza.
Almasi inauwezo wa kusafirisha joto na umeme mara mbili zaidi ya silikoni ambayo ndiyo imekua ikitumika hivyo iwapo almasi itaweza kutengenezwa kwa gharama nafuu itaweza kuruhusu kutumika katika utengenezaji wa vifaa vidogo zaidi vya mawasiliano.
No Comment! Be the first one.