fbpx
Apple, iOS, IPhone

Zawadi ya Dola Milioni 1 kudukua iPhone bado haitazuia udukuzi

zawadi-kudukua-iphone
Sambaza

Kampuni ya Apple imeweka zawadi ya dola milioni 1 kwa mtu atakayeweza kudukua iPhone na kuwapa taarifa ya jinsi walivyofanikiwa kufanya hivyo.

Pesa hiyo ambayo ni zaidi ya Tsh Bilioni 2 zinalenga kuhakikisha wadukuaji hawauzi teknolojia hizo kwa makampuni mengine. Ingawa kwa muda mrefu Apple wamekuwa wakiichukulia sifa ya kuwa iPhone haziwezi kudukuliwa hali imekuwa tofauti hivi karibuni. Kuna makampuni ya kiusalama hasa ya Israel yaliyoonesha tayari kuwa na uwezo huo.

INAYOHUSIANA  App ya Siri yakosea; yatoa majibu yasiyosahihi

iPhone refurbished kudukua iphone

Kwa dau hili wanategemea mtafiti mdukuzi akifanikiwa kuona tatizo au njia ya kudukua iOS au MacOS achukue uamuzi wa kuwapa taarifa hizo Apple na si yeye kutumia taarifa hizo kwa manufaa yake mwenyewe au kuuzia makampuni mengine.

Dau hili la dola milioni 1 za Kimarekani kwa mtu atakayeweza kudukua iPhone au MacBook ni kubwa sana kwani kipindi cha nyuma wamekuwa wakitoa zawadi ya dola laki 2. Uamuzi huu unaonesha kuwafanya wadukuzi kuvutiwa zaidi na kuwapa Apple siri ya mafanikio yao badala ya wao kuyauzia makampuni ya kiusalama kama vile …. kutoka Israel.

INAYOHUSIANA  Miaka 40 ya Apple; Mambo 5 ambayo pengine huyajui

Hivi karibuni imeonekana mashirika ya kiusalama kama vile FBI yapo tayari kulipia huduma hizo pale ambapo msimamo wa Apple umekuwa mara zote kutosaidia kufungua simu za wateja wao.

Kwa kutumia njia hii Apple wanahakikisha ni wao ndio watavutia wadukuzi kuwapa taarifa za njia za kudukua na kuboresha usalama katika programu endeshaji zao za iOS au MacOS. Utaratibu wa zawadi za pesa kwa wadukuzi ambao ni watafiti wa mambo ya kiusalama unatumiwa pia na makampuni mengine makubwa kama vile Google.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |