Apple ni moja kati ya chapa kubwa sana na chapa hii inasifika kwa kuwa na bidhaa na huduma nzuri za kiteknolojia.
Ukiachana na kusifika sana kwa utengenezaji wake wa iPhone bado Apple ina bidhaa zingine nyingi tuu kama vile ujazo uhifadhi wa mtandao na mambo mengine mengi.
Kampuni hiyo nembo yake ni tunda la tufaha (Apple) ambalo limemegwa kidogo, Apple nao wameamua kuifanya alama hiyo ya tufaha katika biashara kuwa ya kwao tuu.
Mfano tuu huko Switzerland Apple wao wamejaribu kuifanya alama hiyo ya tofaa katika biashara kuwa ya kwako tokea mwaka 2017 na ukiachana na huko wamefanya hivyo pia katika nchi zingine kadhalika.
Huko huko Switzerland kuna kampuni ina miaka 111 (The Fruit Union Suisse) na kwa sasa inaweza ikaenda mpaka kubadilisha nembo yake kwa sababu ya Apple
Wao Fruit Union Suisse wamelalamika kwa hatua hiyo ya kutaka kumiliki nembo ya tufaha (tunda) kwa nembo hiyo ni ya duania nzima na kama wakifanya hivyo makampuni mengi duniani yataathirika.
Kingine ni kwamba mpaka sasa bado hatua hii haijafanikiwa kwa asilimia 100 maana bado mambo yapo katika mchakato endelevu.
Fruit Union Suisse yenyewe tuu imepinga swala hilo kisheria –kesi inaendelea– huku wenzao nao wamekua wakipambana nao jino kwa jino.
Wengi wanajiuliza kwa nini mpaka sasa Apple wanafanya hivyo licha ya wao kuwa na historia ya kufanya hivyo (kumiliki tunda la Apple katika logo)
Wengi wanasema kama ingekua katika vifaa vya kompyuta au hata App ambazo zinatumia logo hii lakini sio wao kwenda mpaka katika makampuni ya kawaida ambayo yanatumia tunda la tufaha.
Hii Ina Maana Gani?
Kwa namna moja au nyingine kampuni inataka alama hiyo ya tunda la tufaha liwe linatumika na wao tuu katika swala zima la biashara/kampuni.
Kinachofanyika ni kwamba Apple inafanya hivyo makusudi ili makampuni mengi –pengine ya matunda—kuweza kubadilisha nembo zao ambazo zina tunda la tufaha.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la maoni, je unadhani ni hatua nzuri kwa Apple kutaka wao ndio wawe wanatumia tunda hilo katika nembo yao tuu?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.