Ukaichana na WhatsApp kuwa juu bado inazidi washangaza watu kwa kuongeza vipengele kadha wa kadha kila siku.
Kipengele kinachosubiriwa kwa hamu na watumiaji wa mtandao wa WhatsApp ni kipengele amacho kinafanana na kile katika mtandao wa Snapchat.
Kwa kupitia kipengele hichi basi watu wanaweza wakatumiana ujumbe mfupi kwa njia ya video kupitia katika mtandao huo.
Ni wazi kwamba WhatsApp ni moja kati ya majukwaa maarufu kabisa kwa kutoa huduma ya kutuma na kupokea meseji za papo kwa papo.
Kipengele hiki kinafahamika sana katika mtandao wa Snapchat lakini kwa haraka haraka ni kwamba hakitakua na tofauti kubwa na kile cha kutuma ujumbe wa sauti (VN).
Cha kufanya kitakua ni kushikilia kitufe cha kamera kisha kuanza kutekodi video fupi na ukitoa kidole (kuacha kurekodi) ndipo video hiyo itamaliiza kujirekodi tayari kwa kutumwa kwa muhusika.
Ili video hizo kutofautishwa na zingine hizi zimekua ni za muda mchache sana ukilinganisha na zingine maana hizi zitaweza kurekodiwa mpaka sekunde 60 tuu.
Uzuri wa hiki kipengele ni kwamba kitakua na msaada mkubwa kama unataka kurekodi kitu na kukituma kwa haraka bila ya kutoka nje ya App ya WhatsApp.
Kipengele hiki bado kitakua kinatawaliwa na teknolojia ile ile ya End-To-End Encryption ambayo inafanya mawasiliano hayo kuwa siri ya watu wanaowasiliana tuu.Kwa sasa kipengele hiki kinapatikana kwa WhatsApp ya majaribio (toleo la Beta) lakini ndani ya wiki za usoni kitaanza kupatikana kwa wote.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani kipengele hiki ni kizuri kwa sasa au kilikua hakina tija?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.