fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Mtandao wa Kijamii whatsapp

Mpya WhatsApp :Mafaili Makubwa, ‘Emoji Reaction’ Na Watu Hadi 512 Katika Group Moja!

Mpya WhatsApp :Mafaili Makubwa, ‘Emoji Reaction’ Na Watu Hadi 512 Katika Group Moja!

Spread the love

WhatsApp na yenyewe inazidi kujiongeza katika kuhakikisha inapambana na mitandao mingine mingi ya kijamii ili izidi kuwa namba moja.

Katika toleo jipya imeongoza vipengele vikubwa vitatu ambavyo mwanzo hatukuvitarajia kuja hivi karibuni naweza kusema

  1. Uwezo wa kuweza kutuma na kupokea mafaili makubwa kupitia WhatsApp

Kwa sasa unaweza kutuma mafaili yenye ukubwa hadi wa GB 2 kitu ambacho mara ya kwanza kilikua hakiwezekani kwa uwezo huo ulikua ni mpaka kufikia MB 100 tuu.

     2. Uwezo Wa Kutumia ‘Reaction’ Kwa Kutumia Emoji Kama Njia Ya Kujibu Jumbe

WhatsApp Reaction

WhatsApp Reaction

Kwa kawaida tunaweza pokea jumbe na kisha tukaijibu kwa kutumia emoji sio? ..

…Hii haina tofauti kubwa hapa kinachofayika ni kwamba badala ya kujibu kabisa utaweza toa hisia zako juu ya jumbe hizo kwa kutumia ’emoji reaction’.

SOMA PIA  Uwezo wa kuwasiliana na WhatsApp moja kwa moja

    3. Uwezo Wa Kuongeza Hadi Watu  512 Katika Group Moja

Si unakumbuka mwisho wa washiriki katika kundi moja la WhatsApp ilikua ni mpaka kufikia idadi ya watu 256?  Ongezeko kubwa kubwa limefanyika sasa ni hadi watu 512.

Kumbuka vipengele hivi vyote vinakuja katika toleo jipya kabisa la WhatsApp hivyo hakikisha una toleo jipya kabisa ili kuweza kufurahia huduma hii.

SOMA PIA  Snapchat yainunua kampuni iliyotengeneza Bitmoji.

Niandikie hapo chini ya comment, je toleo hili litabadilisha chochote juu ya uzoefu wako wa kutumia mtandao wa kijamii wa WhasApp au hakuna kitakachobadilika?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

  Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania