fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
apps Mtandao wa Kijamii TikTok

TikTok Kuanza Kugawana Mapato Ya Matangazo Na Wazalishaji Wa Maudhui (Content)!

TikTok Kuanza Kugawana Mapato Ya Matangazo Na Wazalishaji Wa Maudhui (Content)!

Spread the love

Ni wazi kuwa mitandao mingi inatengeneza pesa kupitia matangazo na mara nyingi tumeona kuwa sehemu ya mapato hayo wanayopata hugawana na wazalishaji wa maudhui.

Hii ni kama mtandao wa YouTube ambao unajulikana sana unavyofanya katika kulipa wazaishaji wa maudhui katika mtandao huo. TikTok nayo imeona isibaki nyuma kabisa.

TikTok

TikTok

Wengi wameipongeza kampuni kwa jambo hili kwani wengi wanaamini ni njia sahihi na ni moja wapo ya njia ambayo itaufanya mtandao kupata wazalishaji maudhui wengi zaidi.

TikTop imesema kupitia mtandao mpya wa TikTok Pulse, ambao kwa haraka haraka utaruhusu matangazo kutokea katika baadhi ya video katika mtandao wa TikTok.

Ili mzalishaji wa maudhui (content creator) kuweza kupata sehemu ya mapato inabidi awe na wafuasi wasiopungua 100,000 kama sehemu ya video zao zikichaguliwa kuonyesha matangazo hayo.

Muoenkano Wa Ndani Wa TikTok (Mfano)

Muoenkano Wa Ndani Wa TikTok (Mfano)

TikTok Pulse itaziduliwa rasmi mwezi wa sita huko na wakwanza kutumia akiwa ni marekani huku masoko mengine yakifuata.

SOMA PIA  Bofya Kupata Toleo Jipya la WhatsApp Plus

Ningependa Kusikia Kutoka Kwako, Nipe Mtazamo Wako Hii Umeipokeaje?

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii

  Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi.
Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania