Twitter ni mtandao wa kijamii ambao ni mkubwa sana na wenye hadhi ya kipekee. Mtandao huu unatumika kwa mambo mengi sana lakini kubwa sana ni chombo cha mawasiliano sio?
Ukiachana na hayo mtandao huu umekua na mabadiliko mengi baada ya kumpata boss mpya ambae ni Elon Musk na aliinunua Twitter kwa mabilioni ya dola.
Baadhi ya mabadiliko ambayo amekuja nayo ni kama kubadilisha mfumo wa mtandao huo, kubadili vipengele na vile vile hata kubadili na kupunguza wafanyakazi.
Ni wazi kuwa kuna taarifa aliitoa kwamba kila mtu anaweza akapata tiki ile ya blue (verified) lakini ili mtu wa kawaida kabisa kuwa nayo inabidi ailipie.
Kingine ambacho hakifichiki ni kwamba makampuni mengi ya simu yanafanya haya ili kuhakikisha kuwa yanakua na vyanzo vingi vya mapato.
Swala la tiki ya bluu kutoka Twitter ni kwamba wao wanasema kabisa kuna watu wa kawaida, watu wa serikali na watu ambao ni maarufu kama vile wasanii n.k
Kwa kawaida bwana Elon anasema watu hawa hawawezi kuwa sawa jambo ambalo kwa mara ya kwanza halikua na utofautisho katika mtandao wa Twitter maana wote walikua wanapewa tiki ya bluu
Kwa sasa kutakua na tiki za aina tatu –ambazo zinatolewa na mtandao huo
Tiki Ya Gold: Hii ni kwa ajili ya makampuni
Tiki Ya Kijivu: Hii ni kwa ajili ya viongozi wa kiserikali
TIki Ya Bluu: Hii ni tiki kwa ajili ya watu wa kawaida, lakini hii ni kwa watumiaji wa Twitter Blue
Sorry for the delay, we’re tentatively launching Verified on Friday next week.
Gold check for companies, grey check for government, blue for individuals (celebrity or not) and all verified accounts will be manually authenticated before check activates.
Painful, but necessary.
— Elon Musk (@elonmusk) November 25, 2022
Bwana Elon kwa maono yake ni kwamba anataka kuufanya mtandao wa Twitter kuwa ni moja kati ya mitandao ya kijamii ambayo iko tofauti sana na mingine
Lakini ukaichana na vipengele hivi ambavyo vimeandaliwa kuna watu kama vile wasanii wakubwa na watu wengine wenye majina makubwa watakua na uwezo wa kupata tiki hizo bila hata ya kulipia.
Kulipia kumewekwa ili kila mtu ambae anataka kuwa na tiki hiyo basi ainunue. Kumbuka kwa sasa huduma ya Twitter Bluu inapatikana kwa kiasi cha dola 8 za kimarekani.
Kingine kuzuri ni kwamba katika moja ya mabadiliko ambayo yanafanya mtumiaji wa Twitter atakua na uwezo wa kuonesha ni sehemu gani anafanyia kazi au anajihusisha napo.
Hiyo sehemu itatokea pembeni ya tiki yake (bluu, gold au kijivu) lakini cha msingi ni kwamba inabidi kampuni ambayo anasema anafanyia na yenyewe iidhinishe jambo hilo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je unadhani mabadiliko haya kwa mtandao huu yana tija? Au mambo ni mengi, muda ni mchache?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.