Ukiachana na kuwa hawa jamaa (Apple na Samsung) ni washindani wakubwa sana katika soko bado wanakua ni washirika ambao wanafanya biashara pamoja.
Ni wazi kuwa kampuni ya Apple inatumia vipuri vingi kutoka katika makampuni mengine mengi tuu. Moja ya makampuni hayo ni Samsung ambao wameshawahi kuwauzia chip za simu zao na sasa ni zamu ya vioo kwa iPhone 14.
Ukiachana na chip hizo kwa sasa Samsung inawauzia Apple vioo tena vile vya teknolojia ya OLED na vioo hivi ni mahususi katika matoleo ya iPhone 14.
Ni wazi kuwa jambo hili sio geni sana masikioni mwa watu sio? Lakini kingine cha kutilia maanani ni kwamba kampuni ya Samsung ni moja kati ya makampuni inayoongoza katika soko la kuuza vioo vya OLED.
Kwa taarifa zilizopo ni kwamba kampuni ya Samsung itasambaza asilimia 70 ya vioo vya OLED kwa iPhone 14 zote.
Taarifa zingine zilizopo ni kwamba Apple ina mpango wa kuzalisha matoleo ya iPhone 14 yapatayo milioni 120 ukiachana na hayo angalau milioni 80 zitakua zinatumia vioo vya OLED kutoka Samsung.
Idadi ya vioo vilivyobaki vitapatikana kwa makampuni mengine kama vile LG.
Samsung imekua ikipata sifa kadha wa kadha katika vioo vyake na ukizingatia simu kama Samsung Galaxy S22 Ultra imesifiwa sana kuhusiana na kioo chake.
Ifahamike ili simu ya iPhone ikamilike kabisa basi ni lazima vifaa mbalimbali kutoka katika makampuni mbalimbali viunganishwe na Apple.
Ushindani na kufanya kazi kwa wakati mmoja pengne ndio jambo ambalo linawafanya Apple na Samsung kufanikiwa sana na kuendelea kuwa katika nafasi za juu sana katika soko.
Chanzo: GSMArena
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je hii umeipokeaje? Unadhani ni sawa kwa kampuni kama Apple kwenda kununua vifaa kwa Samsung haswa kwenye toleo lake la iPhone 14?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.