Kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu, Vodacom, imeandaa shindano kwa ‘developers’ katika nchi za Africa na Uarabuni kuweza kutengeneza, kuuza na hatimaye kushinda zawadi mbalimbali kutokana na mawazo yao na app watakazotengeneza.
Kupitia shindano hili, wataalamu wa teknolojia wanaoishi na kufanya kazi katika nchi za Tanzania, Afrika Kusini, Misri, Lesotho na Qatar watapata nafasi hii ya kipekee katika kuamsha, kuchochea na kuendeleza vipaji na sekta nzima ya teknolojia katika nchi hizi.
Katika dunia ya sasa ambayo tunaona ukuaji wa matumizi ya vifaa vya elektroniki kama simu, tableti na kompyuta ambazo zinaitaji apps/programu nyingi zaidi kwa ajili ya mahitaji mbalimbali ya jamii tofauti tofauti, bila ubishi kunafunguka soko zuri na chanzo cha ajira katika sekta ambayo nchi zetu zimekuwa nyuma kidogo.
Naamini kupitia shindano hili muda umefika wa kuona watanzania wakiajiriwa au kujiajiri kwa viwango vya kama Zynga au kuja na apps maarufu viwango vya Angry Birds.
Kama kipaji unacho au kuna mtu unayejua anakipaji katika mambo haya basi muda ndio huu, unaweza kupata habari zaidi na kujiandikisha kupitia mtandao wao wa www.vodacomappstar.com
No Comment! Be the first one.