Alivyosasa |
Zamani |
Muongozaji filamu maarufu Marekani wa filamu iliyofanya vizuri zaidi duniani ya Matrix, amekuwa mtu maarufu zaidi duniani kubadilisha jinsia yake.
Director huyo kwa sasa ambaye amebadilika kuanzia sura na maumbile mengine anafahamika kwa jina jipya la Lana Wachowski kutoka lile la zamani ambalo lilikuwa Larry Wachowski.
Lana Akijificha Kutoka Kwa Waandishi wa Habari |
Ameonekana zaidi baada ya kuanza kutangaza filamu mpya aliyo’direct na kujitangaza kwa kutumia jina lake hilo jipya. Filamu hiyo inatambulika kama “Cloud Atlas“,ni ya sayansi ya uongo (science fiction) na imechezwa na nyota Tom Hanks na Halle Berry.
Miaka michache nyuma baada ya kutoa filamu ya Matrix muongozaji filamu huyu alitengana na mke wake na watu wengi walidhani anamuacha kwa ajili ya mwanamke mwingine ila sasa imeonekana kuwa alikuwa ‘amechoshwa’ kuwa mwanaume.
‘Trans-Gender’-Ni Kitu Gani?
Kutoka Mwanamke hadi Mwanaume |
Watu ambao wamezaliwa katika jinsia flani na wamejikuta kujiona tofauti sana jinsia hiyo, wakiwa na mitazamo, na kitabia za jinsia nyingine na kuchukua uamuzi wa kujibadilisha kabisa kuanzia mavazi na pamoja na kutumia homoni za jinsia nyingine zinazotengenezwa kwenye maabara (artificial hormones) na kumalizia hatua ya mwisho ambayo ni kufanya upasuaji wa kubadilisha maumbile (Genital Reassignment Surgery) huwekwa kwenye kundi la ‘Trans-Gender’.
Watu hawa wapo takribani 700,000 nchini Marekani kwa data ya mwaka jana kutoka chuo cha Williams (Williams Institute – UCLA School of Law) , nchini Marekani.
Na sheria ya taifa la Marekani linawatambua kisheria, na inasemekana kuna maelfu ya watu wanafanya maamuzi ya kujibadilisha kila mwaka na wengi wao ni wale ambao wamechosha na kupewa jina la kuwa shoga (gays) hivyo wanaona jamba la mwisho ni kujibadilisha kabisa! Kazi ipo!!!!
Kiukweli ukilitazama jambo hili kwa undani utajiuliza ni vingapi vinashindikana katika sayansi kwa ulimwengu wa sasa. Kitu kimoja tuu kimebaki nacho ni kuweza kukishindwa kifo…
Mtazamo wako ni upi katika hili?
No Comment! Be the first one.