fbpx

Pepsi wana mpango wa kuja na matangazo ya angani!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Makampuni makubwa hayawezi kuacha kutangaza bidhaa zake, lakini pia mara zote hutafuta njia za kujitangaza kitofauti zaidi. #Pepsi wapo njiani kuweka matangazo ya kinywaji chao kimoja juu kwenye anga

Makampuni haya yana tabia ya kutumia pesa nyingi sana katika matangazo japokuwa kwa kiasi kikubwa bidhaa zake zinajulikana.

Sasa basi hebu fikiria pale jua likizama alafu unaona tangazo la kampuni fulani, hii itapendezesha anga sana, mpaka jua lichomoze tena anga itakua imejaa na kivutio/vivutio vya aina yake.

Kampuni Ya Kufikirika --LocaCola-- Ikiwa inatengazwa Angani

Picha ya mfano wa jinsi matangazo yatakuwa yanaonekana angani

Kampuni ya urusi ambayo inaitwa StartRocket kwa ushirika na kampuni la Pepsi wameonyesha nia katika kuhakikisha wanalifanikisha jambo hili. Hii ni aina nyingine kabisa ya matangazo na inawezekana wakawa ndio wa kwanza kuja na tangazo la aina hii.

INAYOHUSIANA  Tuangalie Maboresho Katika App Ya SnapChat!

Kumbuka matangazo haya yatakuwa yanarushwa na satelaiti maalum huko angani. tayari teknolojia hii iko katika mchakato.

Ijulikane pia kuwa matangazo ya aina hii yataleta mapinduzi makubwa sana katika teknolojia hasa katika swala zima la makampuni mbali mbali ya kutangaza. kampuni halijaongea mambo mengi sana kuhusiana na jambo hili.

Bado kuna wengine wanahisi jambo hili bado haliwezi kuwezekana na kwamba kampuni Ya Pepsi linafanya kiki tuu ili tuu watu waiongelee … tazama tweet hizi.

Logo ambayo inaonekana katika picha ni logo ya kampuni ya kufikirika ambayo inaitwa LocaCola

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini. wewe hili umelipokeaje je unahisi hili ni jambo zuri na ni njia sahihi ambayo makampuni inabidi yatumie katika kujitangaza

Tembelea TeknoKona kila siku, ili kujipatia habari kede kede za kiteknolojia. Kumbuka  daima tupo nawe katika teknolojia.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.