Threads ni mtandao ambao hauna muda mrefu sana na umalikiwa na kampuni ya Meta ambao inamiliki mitandao ya Facebook, Instagram na WhatsApp.
Threads inaonyesha ukuaji mkubwa huku mtandao wa x (zamani twitter) namba zikionyesha kuwa mtandao huo unasua sua.
Threads katika soko la App la App Store iko namba 4 na namba nane katika soko la app la Google Play Store.
Kwa sasa mtandao wakijamii wa Threads umefikia watumiahi milioni 130 kwa mwezi tena wale ambao wanatumia mtandao huo mara kwa mara.
Moja kati ya kitu ambacho kilishangaza wengi sana ni mwanzoni mtandao huu ulivyoanzishwa na kupata namba nyingi ya watu ambao wanajiunga na kisha namba hizo kuanza kupanda taratibu zaidi.
Kumbuka kwa kipindi cha siku tano tuu mtandao wa Threads ulikua umefikisha idadi ya watu 100 ndani ya siku hizo pekee na wengi wakitabiri kuwa namba hiyo itapanda maradufu.
Mtandao wa X ambao zamani ulijulikana kama Twitter umeonyesha dhahiri kushuka kwa kiwango cha kushushwa na watu.
Kumbuka kwa mwezi julai mwaka jana mtandao huu ulikua na watumiaji milioni 540 kwa mwezi ambao wanatumia mtandao huo mara kwa mara.
Upandaji wa namba hizi mbili kwa mtandao wa X zimeonekana zikiwa zinasua sua sana kwa mfano mzuri ni kwamba mwezi disemba 2023 ilikua namba 36 katika soko.
Kwa namba hiyo pengine labda haikushtui lakini ukifikiria sana ni kwamba ni namba mbaya maana mtandao huo uko tangia mwaka 2006.
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.