Username ni kitu cha kawaida kabisa katika mitandao ya kijamii na ndio kinachotumika kututambulisha, huduma kama hii inatumika hata katika mtandao wa Telegram, hivyo basi na WhatsApp wameona wasibaki nyuma.
WhatsApp licha ya umaarufu wake wote ilikua haijaanzisha kipengele hichi cha kutumia Username, mpaka sasa watu wanatambuana kwa kutumia namba za simu ndani ya mtandao huo.
Kingine cha kutilia maanani ni kwamba kama huduma hii ikifika katika mtandao huu wa kijamii basi hata usalama na ulinzi wa faragha utaongezeka kwa kiasi ndani ya mtandao huo.
Pata picha katika makundi (group) hii inaamanisha itakua ni vigumu sana kwa taarifa zako kama vile namba kukaa wazi itatokea username yako.
Kingine ni kwamba kama umekutana na mtu na unataka kuwa uwe unawasiliana nae katika mtandao huo itakua haina ulazima wa wewe kutoa namba yako ya simu kwani tayari utakua na Username.
Ni wazi kabisa kwamba Meta wamesanuka kwamba kuna uwezekano mkubwa sana watu wanapendelea kuongeza baadhi ya watu katika WhatsApp zao bila ya kutegemea namba za simu.
WABetaInfo imeweka wazi kwamba toleo hilo liko njiani na kwa sasa liko katika hatua za mwanzo mwanzo kabisa.
Kingine kizuri ni kwamba bila namba unaweza kumtafuta mtu na kuweza kuongea nae ingali una Username yake tuu.
Kipengele hiki kwa sasa kipo katika hatua za mwanzo mwanzo kabisa na kikikamilika kitatoka kwa watumiaji wote duniani.
Mara kwa mara WhatsApp imekua ikiongeza vipengele kadha wa kadha katika huduma yake ili kujihakikishia inabakia kuwa juu zaidi ya zile zingine
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, je udhani kipengele hiki ni kizuri au hakina maana sana kwa sasa?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.