WhatsApp ni moja kati ya mitandao ya kijamii mikubwa sana na yenye watumiaji wengi sana licha ya ukubwa wake bado ni njia rahisi kabisa ya mawasiliano kwa wengi tuu.
Mtandao – WhatsApp — bado unaleta vipengele vipya mara kwa mara na licha ya hivyo bado mtandao unahakikisha kwamba vipengele ambavyo vipo vinapata maboresho.
Nadhani umeshawahi piga na kupokea simu za video katika mtandao huo, hapo mara ya kwanza ulikua huwezi kutoka katika mtandao huo na kuendelea kufanya mambo mengine wakati simu hiyo ikiendelea sio?
Na kama ukifanikiwa kutoka basi mara nyingi huwa upande wa pili –unapowasiliana napo—wanakua wanaona giza tuu, hawakuoni wewe?
Kwa sasa kwa watumiaji wa iPhone jambo hili linaenda kuisha kabisa kwani kwa kutumia teknolojia ya Picture-in-Picture litakamilika
Uwezo wa kuwa katika simu ya video huku ukawa unafanya mambo yako mengine katika kifaa cha iPhone utawezekana na vile vile hata upande wa pili utakua unakuona vizuri.
Taarifa hizi mwanzoni kabisa zimetolewa na mtandao wa WABetaInfo na kwa sasa kipengele hiki kipo katika majaribio na kitaanza kupatikana kwa watumiaji wote wa iPhone hivi karibuni.
Uzuri wa kipengele hiki ni kwamba unaweza hata ukatoka kabisa katika mtandao wa WhatsApp na bado ukawa unaendelea na simu yako ya video.
Licha ya hayo kuna kwa baadhi ya vifaa vya iPhone huduma hii imeshaanza kuwafikia, kama kwako bado hakikisha una toleo la juu kabisa la WhatsApp au kuendelea kusubiria
Soma Kila Kitu Kuhusu WhatsApp >>HAPA<<
WhatsApp umekua ni moja kati ya mitandao ya kijamii ambayo ina masasisho mengi sana katika kuhakikisha kuwa inawaletea watumiaji wake kile kilicho bora kabisa.
Chanzo: WABetaInfo.
Ningependa kusikia kutoka kwako, naindikie hapo chini katika eneo la comment, je hili umelipokeaje? Ulishaanza kutumia kipengele hiki au bado hakijakufikia?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Wa TeknoKona Kila Siku, Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.