Je huwa unatuma ujumbe flani na ndani ya dakika chache tayari unagundua umefanya hivyo kimakosa? Whatsapp kuja na uwezo wa kufuta ujumbe uliokwishatumwa.
Katika toleo la beta la simu za iOS (lililokwenye mtengenezo) kwa sasa la app hiyo maarufu uwezo huo unaonekana katika eneo la ‘settings’.
Kikubwa ni kwamba utaweza kufanya hivyo kama tuu mtumiaji mwingine bado hajausoma ujumbe huo. Kama ukishasomwa basi hautaweza ufuta tena.
Uwezo huo utafanyaje kazi?
Ukishatuma ujumbe basi utaweza kubofya na kuendelea kushikilia kwenye ujumbe huo ulioutuma na utapata mapendekezo mawili. ‘Edit’ yaana fanya maboresho au ufute – ‘revoke’.
Hadi sasa WhatsApp wenyewe hawajatoa taarifa rasmi juu ya lini uwezo huo utakuja kwa watumiaji wote wa WhatsApp. Kikubwa ni kwamba ni kitu ambacho tukitegemee kuja katika toleo lolote jipya kwa sasa.
Je wewe ni mtumiaji wa WhatsApp? Unaona kuna umuhimu wa kiasi gani wa uwezo huu?
Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTube, Telegram na Google Plus
Vyanzo: Tovuti mbalimbali
One Comment
Comments are closed.