Moja ya matukio makubwa ambayo yamefanyika Mwezi huu wa Mei ni uzinduzi wa simu mpya aina ya TECNO Camon 20 Premier.
TECNO Camon 20 Premier imekuwa gumzo tangu kuzinduliwa kwake na miongoni mwa sifa (feature) ambayo imeonekana kuvutiwa wengi ni muundo mzima (muonekano) wa simu na mali ghafi na ubunifu uliyotumika sehemu ya nyuma ya simu hizo.
TECNO imezichanga vyema karata zake, imeweza kubadili muonekano mzima wa simu za TECNO na si kama ambavyo tumezizoea.
Teknolojia ya Magic Skin na Ceramic kuna itambulisha upya TECNO katika ulimwengu wa simu janja kuwa Kampuni nambari moja ya simu yenye kupokea mabadiliko ya teknolojia kwa haraka.
Enheee, kabla sijaizungumzia Megapixel 108+50+2 za camera ya nyuma naomba kwanza TECNO ipewe Maua yake kwa ukomavu mkubwa wa kutambulisha teknolojia ya RGBW pro katika simu hii
Kama ilivyo kwa Samsung kuongeza uwezo wa upigaji picha ang’avu zaidi kulingana na size ya pikseli na kuonesha kilichopo kwa udogo kwa rangi yake halisi, hii imerudisha matumaini makubwa kwa wadau wa simu za TECNO.
TECNO Camon 20 Premier inapatikana kuanzia sh.400,000/=
Mabadilko mengi yamefanywa na TECNO ikiwemo muonekano wenye hadhi ya kisasa, camera kama ambavyo nimesema hapo awali lakini cha kufurahisha zaidi kampuni hii haijabadilisha utamaduni wake wa kumjali mteja wake kupitia bei.
Kingine na kujua kama kampuni hii inakua kwa haraka sana, fikiria simu yako ya kwanza ya TECNO ambayo uliwahi iona/itumia alafu fananisha na mabadiliko ambayo yapo mpaka sasa? umegundua kitu sio?
Nifuate Kwenye Mitandao Yangu Ya Kijamii
Instagram | Facebook | Twitter | LinkedIn
No Comment! Be the first one.