Kutokana na mlipuko wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona aina ya COVID-19 makampuni mengi yameyumba kiuchumi lakini wenyewe Apple wameendelea uundaji wa iPhone 12 ambayo inatazamiwa kutoka machoni pa watu baadae mwaka huu.
Moja ya bidhaa ambayo hivi sasa inazungumziwa kwenye tovuti mbalimbali ni iPhone 12 kuhusiana na fununu mbalimbali zinazohusu rununu husika; muonekano wake wa mbele na nyuma umeshaanza kufahamika.
Kuna miezi sita au zaidi mpaka toleo lingine la iPhone liweze kutoka lakini kuna habari ni fununu kuhusu ujio wa simu janja ijayo kutoka Apple na ikionekana vile vitu vyote ambavyo tumezoea kuviona kwenye uso wa mbele vikiwa sambamba na kioo sasa vinaonekana kwa juu kabisa kabla ya yote.

Vilevile, simu hizo zinatazamiwa kuwa na urefu wa inchi 6.1 (iPhone 12), inchi 6.5 (iPhone 12 Pro) na inchi 6.7 (kwa ile ya Pro Max) kwenye kioo, RAM GB 6 na kuonekana kuwa na umbo pana kidogo kuliko toleo la nyuma. Sehemu ya kuweka kadi ya simu inaonekana kutobadilika na kuendelea kuwepo upande wa kulia. Pia, teknolojia ya 5G inazungumzwa kuwepo kwenye simu hiyo ijayo jambo ambalo linaendana na teknolojia ya intaneti duniani.

Kuna mengi tuu ambayo tutaendelea kuyasikia mpaka pale ambapo Apple watatoa simu hiyo na kuweza kupata hakika ya kile ambacho tulikuwa tunasoma kwenye mitandao mbalimbali au ni tofauti kabisa na ambacho kilikuwa kimeshafamika. Inatubidi tuu tuvute subira mpaka itakapozinduliwa.
Vyanzoi: GSMArena, Forbes