Simu janja tunazonunua tufahamu ya kuwa huwa zinaangaliwa ili kuzikinga na mambo mabaya amabayo yanaweza kuleta/kusababisha athari kwa yule anayeitumia. Vilevile, zoezi hilo huwa linakuwa ni kwa muda fulani kisha baada ya hapo unasitishwa.
Ukiwa kama mfutialiaji mzuri wa habari zinazohusu Samsung nikirudi nyuma mpaka mwezi Juni mwaka huu utakuwa ulisoma mahali kuwa Galaxy S7 na S7 edge hazipo kwenye mpango wa kuendelea kupokea masasisho ya ulinzi hivyo basi zikawa zimewekwa kwenye kundi la rununu zitakazopokea masasisho mengineyo.
Lakini sasa kulingana na taarifa liyotoka siku chache zilizopita imebanika kuwa simu janja tajwa zimerudishwa kwenye orodha ya zile simu janja za Samsung zinapokea masasisho ya kiusalama kila robo ya mwaka mpaka hapo itakapoamuliwa vinginevyo. Swali ni je, kwanini kampuni hiyo kubwa iliamua kuziweka kando simu hizo kupokea masasisho muhimu kabisa? Rununu husika zilizinduliwa zaidi ya miaka mitatu (3) iliyopita na ni kawaida kwa makampuni ya teknolojia kusitisha huduma fulani fulani kwa vifaa vyenye umri wa miaka mitatu au zaidi sokoni.

Zipo simu janja za Samsung ambazo zenyewe zinapokea maboresho ya kiulinzi kila baada ya miezi minne kupita kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini. Pia, kuna zile ambazo zinapokea masasisho ya aina niliyoisema kila mwezi na simu hizo ni Galaxy A5 (2017), Galaxy A8 (2018), Galaxy S8, Galaxy S8+, Galaxy S8 Active, Galaxy S9, Galaxy S9+, Galaxy S10, Galaxy S10+, Galaxy S10e, Galaxy S10 5G, Galaxy Note 8, na Galaxy Note 9.

Kwa wanaotumia simu hizo na wanaojua umuhimu wa masasissho nina hakika watakuwa wamefurahishwa na habari hii. Sasa kazi ni kwako wewe kuwa tayari kuyashusha mara tu yanapopatikana.
Vyanzo: GSMArena, Android Central