Uamuzi wa kujitoa Umoja wa Ulaya unaifanya Uingereza kufikiria kila namna ambayo itawasaidia wao baada ya kukamilisha mchakato mzima wa kujiondoa kutoka kwenye umoja huo miezi kadhaa ijayo.
Mwaka 2003, Umoja wa Ulaya iliridhia ujenzi wa satelaiti kwa matumizi ya pamoja inayofahamiika kama Galileo ambayo inatarajiwa kukamilika mwaka 2020 na ikigharimu Euro 10bn|$11.44bn.
Kwanini Uingereza inataka kujenga satelaiti ya kwake mwenyewe?
Hatua hiyo imefuatia baada ya mpango wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya na kuelezwa kuwa kama nchi itaruhusiwa kutumia Galileo kupitia chaneli ya wazi lakini jeshi la nchi hiyo litadhibitiwa kwa kiwango fulani kuweza kutumia kifaa hicho huku tangu ujenzi wa satelaiti hiyo serikali ya Uingereza imechangia.
Sasa katika nia ya kuondoa mtafaruku kati ya Umoja wa Ulaya na Uingereza, kama nchi imeamua kujenga satelaiti ya kwake mwenyewe kwa ajili ya tafiti mbalimbali.