fbpx
Panasonic, simu, Teknolojia

Gharama za vioo vya OLED kupungua

gharama-za-vioo-vya-oled-kupungua
Sambaza

Makampuni mengi yamekuwa yakiachana polepole kutumia vioo ya LCD na kuhamia kwenye teknolojia ya OLED lakini daima gharama za vioo hivyo imekuwa ipo juu jambo ambalo linasababisha hata bidhaa kamili kuwa ghali.

Panasonic imeliona suala hilo na kuamua kuchukua hatua ambayo itapunguza uwekezaji kwenye teknolojia hiyo; ilichokifanya kampuni hiyo ni kuunganisha nguvu (kuingia ubia) na Screen Holdings Co. Ltd.

Panasonic kazi yao itakuwa ni kuchora mchoro pamoja na kuunda kifaa ambacho kitatumika kutoa nakala mbalimbali huku upande wa pili (Screen Holdings Co. Ltd) kazi ikiwa ni kufanikisha uzalishaji wa bidhaa husika pamoja na kufanya matengenezo.

Gharama za vioo
Kioo cha OLED kutoka Panasonic: Ubia huo wa Panasonic na Screen Holdings Co. Ltd utapunguza gharama za utengenezaji wa vioo vya OLED kwa asilimia 20-30.

Teknolojia ya utengenezaji wa vioo ya OLED ilianzishwa na Sony pamoja na Pioneer Corp miaka ya ’90  kisha makampuni mengine yakajaribu kutumia teknolojia hiyo lakini wakaachana nayo baada ya muda kutokana na gharama za uzalishaji kuwa juu.

INAYOHUSIANA  Serikali ya Uingereza yatishia kufungia mitandao ya kijamii

Teknolojia ya kwenye OLED ndio inafanya simu kama iPhone X kuwa ghali sana lakini kwa ushirikiano wa Sony Corp na Panasonic (JOLED) wanatarajiwa kuanza kutoa vioo vya aina hiyo kwa bei nafuu ifikapo mwaka 2020.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , , , ,

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|