Vuta pumzi alafu fikiria, kichwa cha mtu mmoja mzima aliyehai mwenye tatizo na mwili wake wa chini kwa sababu mbalimbali iwe ni ugonjwa kama kansa au ulemavu wa kupooza kikatwe na kuhamishiwa kwenye mwili mwingine ambao ni mzima!
Ndiyo, kitu ambacho washajiuliza mara kadhaa kama kinawezekana na wakakata tamaa ila kuna daktari ambaye amesema kinawezekana na yupo njiani kufanikisha hilo.
Na mtu wa kwanja kujitolea kwa ajili ya oparesheni hiyo ni kijana mmoja wa miaka 30 kutoka Russia mwenye tatizo la kupooza kwa misuli ya mwili kiasi ya kuwa mlemavu kabisa. Kijana huyo aitwaye Valery Spiridonov ambaye anafanya kazi kwenye moja ya kampuni inayojihusisha na masuala ya teknolojia ya mawasiliano nnchini Russia hali inazidi kuwa mbaya mwaka hadi mwaka na hivyo kwa ihari yake mwenyewe amejiingiza katika jaribio hilo.
Mwenyewe amesema anaamini matokeo yoyote baada ya oparesheni ya upandikizaji huo hautamsaidia yeye tuu bali atakama yeye yatampata mabaya basi yataisaidia sayansi na teknolojia hiyo ya upandikizaji wa kichwa na kiwiliwili kwa miaka ijayo.
Pointi muhimu kuhusu oparesheni hii
> Daktari mkuu anayesema ni jambo linalowezekana na ndiyo atakayeongoza katika kufanikisha anaitwa Dr Sergio Canavero, muitaliano.
> Oparesheni hiyo itachukua muda wa masaa 36 na itagharimu zaidi ya Sh bilioni 20 za kitanzania.
> Kiwiliwili (mwili) utakaotumika ni wa mtu ambaye ubongo wake umekufa ila viungo vingine vyote vya mwili vipo katika hali nzuri na ni mwenye afya.
“Wakati wa oparesheni hiyo kichwa cha kijana huyu kitawekwa katika hali kali ya ubaridi wa digrii 10 – 15 kwani katika hali hii chembe hai (cells) zitaweza kukaa hai kwa muda mrefu wakati kichwa kikitolewa na kupachikwa kwenye mwili mpya.”
> Kisu spesheli kilichotengenezwa kwa teknolojia ya juu mahususi kwa ajili ya jambo hili kitatumika katika kukata eneo la shingo bila kufanya madhara yoyote. Kitu kuwa ni chembamba na chenye makali ya hali ya juu – ‘An ultra-sharp scalpel’.
> Baada ya operesheni huyu kijana, Bwana Valery, atawekwa kwenye hali ya ‘koma’ (usingizi mzito) kwa muda wa wiki 3 hadi nne ili kumzuia asisogee wala kutingishika kabisa….asije akashtua eneo lililounganishwa. Pia watamchoma madawa maalumu, ‘Immunosuppressants’ ili kuzuia kiwiliwili (yaani mwili mpya) kukikataa kichwa kipya kilichopandikizwa.
“Baada ya oparesheni hiyo mgonjwa akizinduka baada ya wiki 3 au nne ata weza kuutumia uti wa mgongo, kusogeza kiungo kimoja kimoja taratibu, na pia sura yake itaweza kufanyakazi na sauti yake itakuwa ile ile. Na Daktari anategemea ya kwamba mtu huyo ataweza kutembea ndani ya mwaka mmoja.”
Ingawa Daktari Sergio ni mtaalamu anayeheshimika sana katika kazi zake bado wamejitokeza madaktari wengi wakiponda jambo ili wakisema halitafanikiwa na ni jaribio la kijinga… ‘crazy’.
Ila mwenyewe hajakata tamaa kwani ata wakati oparesheni nyingine za upandikizi kwa mfano wa moyo, miguu na uta ule wa sura uliofanyika kama miaka mitano hivi iliyopita kuna madaktari ambao walisema waliokuwa wanafanya wasingefanikiwa.
Historia fupi ya oparesheni za kwanza za upandikizi (Transplant).
Mwaka 1905 – Ndio oparesheni ya kwanza ya kuhamisha ‘cornea’, sehemu ya jicho, ilifanyika na kuweza kumuwezesha mtu apate kuona.
Mwaka 1967 – ndio oparesheni ya kwanza ya kuhamisha moyo kumpatia mgonjwa mwenye matatizo ya moyo ulinyanyika nchini Afrika Kusini
Mwaka 1998 – Madaktari walifanikiwa kumpandikizia mtu mkono mzima wa kulia ambao sio wake nchini Ufaransa
Mwaka 2010 – Madaktari nchini Hispania walifanikiwa kupandikiza sura kwa mtu ambayo sura yake ilishaharibika. Yaani hapa ni kwamba walitoa ngozi ya uso kutoka kwa mtu mwingine na kumwekea yeye.
Teknolojia inavyozidi kukua ndivyo mengi ambayo yalikuwa yanaonekana hayatawezekana kwenye eneo la matibabu ndiyo yanaonekana kama yanawezekana kutokana na msaada mkubwa kutoka kwenye teknolojia mbalimbali.
Je wewe unadhani aina hii ya oparesheni ni sawa?
Endelea kuwa nasi na utapata taarifa pale oparesheni hii ikifanyika na matokeo yake.
Kumbuka kusambaza kwa wengine nao wafahamu makubwa yanayokuja kwani kwa namna hii nadhani wenye pesa wakizeeka wanaweza kuomba kufanyiwa oparesheni ya namna hii wapate miili ya vijana.
Vyanzo: RT News, NewsScientist na mitandao mingine mbalimbali
One Comment