Samsung ndio kampuni inayoongoza katika kutengeneza simu na kuuza, sio hilo tuu vile vile ina miradi mingine inayofanya vizuri kama vile kutengeneza na kuuza TV na kadhalika.
Kwa haraka haraka ni kwamba Samsung imesema kuwa ina uhakika bado itabaki kuwa namba moja katika kutengeneza simu janja kwa kipindi cha miaka kumi ijayo. ifahamike kwamba Samsung ndio inayoshikilia namba moja kwa miaka kumi sasa kama mtengenezaji wa simu janja ambae anauza sana.
Kwa sasa Apple na Huawei wako nyuma ya Samsung kimauzo na kama ukifikiria kwa makini kidogo ni kwamba kampuni hiyo inaweza kuhimili kuwa namba moja kwa kipindi kingine cha miaka kumi. Hii ni kwa sababu imeshikilia namba hiyo kwa muda mrefu sana.

Kwa matoleo ya simu janja ya Samsung Galaxy S10 inaonyesha ni jinsi gani kampuni imeweka nia katika kuhakikisha inazidi kuwa namba moja.
Mkurugenzi mtendaji wa Samsung, Bw. DJ Koh amesema “Hili litawezekana tuu kwani kampuni kama kampuni inatengeneza simu zenye teknolojia ya hali ya juu. Kwa mfano simu janja kama Galaxy Fold (simu ya kujikunja,ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni) ambayo pia itakua inasapoti teknolojia ya 5G na pia AI (artificial Intelligence)”.

Kujua zaidi kuhusu Samsung Galaxy Fold (ya kujikunja) ingia hapa, ukisha maliza ingia tena hapa, alafu malizia na hapa! 😀
Ijulikane kwamba na wategenezaji wengine hawajalala, kumbuka namba 1 inagombaniwa kati ya Apple na Huawei. Huawei wao walishatoa mipango yao ya hapo mbele katika na mipango hiyo inalega sana wao kuwa namba moja kama watengenezaji na wauzaji wa simu janja.
Ningependa kusikia kutoka kwako, wewe unaonaje? Je, nani atashika namba moja na kumtoa samsung ambaye kwa muda mrefu amekua katika namba hiyo?
Tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku, ili kujipatia habari kede kede zinazohusu teknolojia. Kumbuka TeknoKona, daima tupo nawe katika teknolojia!.