fbpx

Kamera 3 kwenye Samsung Galaxy F

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Katika moja ya biadhaa za Samsung ambazo zinasubiriwa kwa hamu na wateja wa simu janja ni Samsung Galaxy F, herufi “F” ikimaanisha ‘Foldable‘ yaani inayojikunja.

Yapo mengi ambayo yameshafahamika kuhusu simu yenyewe na kwa mwaka 2019 Samsung Galaxy F imebainika itakuja na idadi ya kamera tatu (3) kama ilivyo Samsung Galaxy A7 (2018).

kamera 3

Tegemea kuona kamera tatu zikiwa upande wa nyuma wa simu hiyo ambayo itakuwa na uwezo wa kujikunja.

Pia, inaaminika kabisa kioo kidogo cha simu husika kitakuwa na urefu wa inchi 4.6 na pale itakapokunjuliwa urefu wa kioo husika utakuwa ni inchi 7.3.

kamera 3

Rununu Samsung Galaxy F ilivyo ikitazamiwa kuwa na teknolojia ya 5G.

Samsung wanatazamiwa kutoa Galaxy F kabla ya nusu ya kwanza mwaka 2019 kumalizika lakini kabla ya hapo tutegemee kuiona Samsung Galaxy S10+ ambayo pia itazamiwa kuwa na kamera tatu kwa nyuma.

Vyanzo: GSMArena, India Today

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Ifahamu TV ya 4K Ambayo Inabamba Zaidi Ya HD
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.