fbpx

Samsung Galaxy Fold haitakuwa na sehemu ya kuchomeka spika za masikioni

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Baada ya uzinduzi wa simu yake ya mkunjo, Samsung Galaxy Fold imebainika kwamba simu hiyo haitakuwa na sehemu ya kuchomeka spika za masikioni kama ziliyvo simu zake za matoleo  mengine.

Samsung hawakuweka wazi wala kusema chochote kuhusu Earphone/Headphone Jack, badala yake wamezungumzia mambo mazuri yaliyo katika simu hiyo ya Galaxy Fold.

Earphone/Headphone jack ni ile sehemu yenye tundu la kuingizia spika za masikioni kwa ajili ya kusikilizia muziki masikioni au kuchomeka spika za nje kwa usikivu mkubwa zaidi. Badala yake itatumika USB port kuunganisha spika za masikioni/nje.

Galaxy Fold

Teknolojia ya kisasa kwa ajili ya kuwezeha kuchomeka spika za masikioni kwenye simu janja.

Taarifa za mwishoni mwa mwaka jana zilizoripotiwa na vyombo vya habari vya Korea Kusini vilisema huenda Kampuni ya Samsung ikaondoa sehemu ya kuchomekea spika za masikioni katika simu zake za matoleo yajayo.

Aidha, imebainishwa sasa Galaxy Fold itatumia prosesa ya Snapdragon 855 SoC, pamoja na RAM ya GB 12 diski uhifadhi GB 512. Pia imeeelezwa simu hiyo itamudu mikunjo ya kufunga na kufungua kwa muda wa miaka 5 pengine ndio kunaweza kupatikana udhaifu. Makadirio kwa siku itaweza kumudu mikunjo na mikunjuo ipatayo 100 kwa muda wa miaka 5 mfululizo.

Galaxy Fold

Teknolojia ya simu za kukunja/kukunjua inarudi machoni pa watu ila kitofauti.

Teknolojia ndio hiyo inahama kutoka kizazi kimoja hadi kingine na simu nyingine inayotarajiwa kutokuwa na sehemu ya kuchomeka spika za masikioni ni Samsung Galaxy Note 10.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Samsung Waleta Galaxy S III Mini!
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.