Siku ya jana ilikuwa ni sikukubwa kwa watumiaji wa simu za Apple, pamoja na kuzinduliwa simu ndogo ambayo ina uwezo mkubwa ya SE kulikuwa na uzinduzi wa iPad PRO pamoja na toleo jipya la iOS.
Ebu tuangalie….kwa ufupi
iPhone SE
Toleo hili la simu ya SE ambalo limezinduliwa jana ni toleo ambalo limetengenezwa kwaajiri ya watumiaji ambao hawapendi simu zenye ukubwa kama wa iPhone 6 ama 6s lakini wanapenda uwezo wa simu hizi sa sasa. Soma uchambuzi wa iPhone SE hapa -> Uchambuzi: iPhone SE
Inasemekana kwamba kwa mwaka jana pekee simu za iPhone zenye screen ya inchi 4 milioni 30 zilinunuliwa, hii inapeleka ujumbe wa wazi kwa Apple kwamba kuna watumiaji waaminifu ambao hata baada ya matoleo mapya wao wanaona yale ya zamani ni bora. Apple wameamua kutengeneza simu hii ndogo ya SE kwa ajiri ya wale wateja ambao bado wanapendelea simu zenye skriini ndogo na pia kwa bajeti ndogo (bei).
Suala la usiri wa data (privacy)
Apple walitumia tukio hilo la jana kutangaza mambo mengi kwa mashabiki wake ikiwamo jitihada zao za kulinda mazingira hasa kwa kutumia nishati mbadala lakini pia waliongelea juu ya jitihada zao za kuhakisha kwamba usiri wa watumiaji wao unadumishwa kwa kuongeza encryption ambayo sio habari nzuri kwa vyombo vya usalama kama FBI ambao bado wako katika mzozo na Apple wakiwalazimisha kufungua simu gaidi mmoja.
iOS 9.3
Pamoja na simu hiyo Apple jana walizindua toleo jipya la iOS ambalo limeshakuwa linapatikana kwa watumiaji wao (najua baadhi yenu mmeshalipakuwa) toleo hili limekuja na mambo mengi mapya kama vile researchKit ambayo inawasaidia watafiti kuweza kukusanya taarifa za tafiti mbalimbali pamoja na hizi zipo app nyingine kama hizi kwa ajiri ya huduma za afya na elimu.
Zaidi ya yote ni uwezo wa OS hii kupunguza mwanga kukufanya uweze kulala vizuri pindi utakapoitumia usiku hii ni habari nzuri kwa watumiaji ambao hutumia sana iPhone au iPad zao usiku.
Pamoja na mambo yote iOS 9.3 itakuja na mambo mapya kama carplay ambayo ni app kwaajiri ya kucheza mziki katika magari pia wameleta app ambayo ni kwaajiri ya habari ambayo inaitwa Topnews.
Apple Watch
Ukiacha hayo yote product zingine zilizotambulishwa jana ni saa janja mpya za Apple ambazo zinakuja katika rangi mbali mbali na mikanda yakubadilisha. Na pia bei ya kuanzia imeshuka, kuyoka dola 349 za kimarekani hadi dola 299 tuu.
‘Liam’ – roboti wa kufungua iPhone
Pia Apple wametambulishe roboti spesheli katika kuwasaidia kulinda mazingira kwa kuhakikisha iPhone zisizoitajika ziweze kufungulia vizuri ili kila sehemu/part inayopatikana iweze kutumiwa tena (recycling).