Mji wa Brussels Ubeligiji leo ulishambuliwa na magaidi kwa kulipuliwa mabomu pacha katika uwanja wa ndege na kituo cha treni. Tukio hili limegharimu maisha ya takribani watu 30 huku makumi ya watu wakiwa wamejeruhiwa hali iliyopelekea FB kuwasha Safety check ili kusaidia uokoaji.
Mtandao wa kijamii wa Facebook umeendelea kutimiza ahadi iliyotolewa na mmiliki wake ya kwamba ita washa Safety check iwapo janga lolote litatokea mahala popote duniaani, ahadi hii ilitolewa na bosi wa Facebook kufuatia kuwepo na ukosoaji juu ya kwamba huduma hii iliwashwa kwa tukio la Paris wakati jana yake matukio kama yale yalitokea kwa miji mingine na hakukua na kitu chochote.
Facebook waliwasha huduma hiyo ya Safety check ambayo kwa maana ya kawaida ni kwamba inakusaidia wewe kuweza kuwajuza ndugu zako na marafiki katika facebook kwamba upo salama, huduma hii huwashwa kwa watumiaji ambao wapo katika eneo ambalo tukio janga hilo limetokea na hii inasaidia watu kuwatafuta ambao bado hawajasema kama wapo salama.
Hatujui ni lini Afrika mashariki inaweza kukumbwa na janga na tuka hitaji kuitumia huduma hii hivyo ni wajibu wetu kuielewa jinsi inavyofanya kazi ili pindi tunapokuwa katika uhitaji na wakati mitandao inazidiwa.
Kama bado huelewi jinsi ya kutumia safety check makala hii hapa itakusaidia jinsi ya kutumia, share na marafiki zako nao waelewe juu ya jinsi ya kutumia huduma hii ili wawe tayari kama itahitajika.