Kuna msemo uanaosema, marafiki zangu wa zamani wako facebook, wapya wako Instagram, wa baade wako twitter na wa karibu wako WhatsApp. Msemo huu una maana ya kwamba watu wengi tayari wameichoka Facebook na pengine mtandao huo unaweza kutokomea kabisa kwenye mahitaji yao. Facebook kwa SMS inakuwezesha usikose mambo muhimu kwenye Facebook yako ukiwa kwenye mitandao mingine.
Ukweli ulio wazi ni kwamba Facebook bado ni mtandao wenye watu wengi (karibu watu billion 1.23 kila mwezi. Zaidi ya million 757 kila siku na kwenye simu, watu million 945 kwa mwezi. Pia, tafiti zinasema kuwa ni mtandao unaotumika na watu wenye rika tofauti kwani ni rahisi sana kuanza kutumia. Kwa haya machache na mengine, facebook ina faida zake za kipekee zinazoiwezesha kupambana kama huduma na kama kampuni kuhakikisha watu wanaendelea kuitumia.
WanaTeknokona mnaoitumia Facebook vizuri mnaweza kujua kwamba mtandao huo una mambo mengi ila pengine ulikuwa hujatilia maanani huduma ya Facebook kwa sms ambayo imenifanya mimi kurudi facebook na kuitumia kiufanisi zaidi.
Facebook kwa SMS ina uwezo wa kukutoa mtandaoni – ambapo kuna mambo mengi ya kukuteka akili, na kukuwezesha kutumia Facebook pale kitu cha muhimu sana kikitokea – kama siku ya kuzaliwa kwa mtu unayemjali. Pamoja na hilo, unaweza kupata habari mpya kutoka kwa watu na kurasa unazofuatilia moja kwa moja kwenye simu yako bila intaneti.
Kwa upande mwingine, huduma hii inakuwezesha kuwajulisha ndugu, marafiki na wafuatiliaji wako kuhusu hali yako na mawazo yako muda wowote unapotaka – tena bure kupitia mitandao fulani ya simu. Kwa hiyo, kupitia ujumbe mfupi wa SMS utapata habari za watu na makampuni na uwezo wa kuwajibu haraka zaidi punde kitu kinachokupa hamasa kikirushwa Facebook. Zaidi, utapata kujulishwa punde unapopata rafiki mpya na kuweza kuungana nae kirahisi kwa kutuma sms.
Sio haya tu, bali kuna mengi zaidi. Kujua zaidi kuhusu kutumia Facebook ya SMS, inakupasa utembelee kurasa hii. Inahitaji pia uwe na uwezo wa kutafsiri kupitia kivinjari chako au uwe karibu na mtu mwenye ujuzi na lugha ngeni. Kama wewe ni mjanja zaidi na unataka kuitumia sasa, fuata maelekezo yafuatayo kujiunga na huduma hiyo:
- Bofya iliyopo juu, kulia kwenye ukurasa wowote wa Facebook na chagua Settings
- Bofya Mobile
- Bofya Add a Phone
- Chagua nchi (country) na kampuni ya mawasiliano (carrier) na bofya Next
- Kwa kutumia simu yako, tuma ujumbe mfupi wa herufi “F” kwenda namba, kwa mfano, 15666 (tigo) kupata kodi maalumu ya kukuhakiki kwenye kurasa ya Facebook.
- Rudi kwenye kurasa ya Facebook na Ingiza kodi uliyopata kwenye simu, alafu bofya Next
Namba kwa mtandao wako inaweza kuwa tofauti.
Namba za Tanzania:
Zantel (Part of Etisalat): 15582
Tigo: 15666
BOL : 25532665
Kwa kutumia huduma hii ya Facebook kwa SMS, nimeweza kutumia facebook vizuri kabisa na kirahisi zaidi, na pengine kwa manufaa zaidi. Nimejaribu kutumia huduma hii kupitia mitandao mingine ya Twitter na Google. Twitter inafanya kazi kwa shida kidogo na kwa sasa inaweza kutumika na mtandao wa tigo pekee hapa nchini. Kwa upande wa Google, nilifanikiwa kutumia kwa mtindo wa SMS na huduma ya Kalenda ambayo sasa imesitishwa na Google wenyewe.
Jaribu sasa, pengine na wewe utanufaika, na tujulishe Teknokona kuhusu jinsi unavyotumia huduma zingine za intaneti kwa SMS.
No Comment! Be the first one.