fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania
Android apps

WhatsApp ya Android Yapata ‘Update’: Fahamu Mambo 5 Yaliyoboreshwa

WhatsApp ya Android Yapata ‘Update’: Fahamu Mambo 5 Yaliyoboreshwa

Spread the love

Baada ya muda mrefu wa majaribio, yaani beta, toleo jipya la WhatsApp kwa ajili ya Android laja likiwa na sifa 5 kubwa za maboresho mazuri zaidi. Fahamu vyote vipya kupitia mtandao wako wa TeknoKona.

1. Soma alafu fanya ujumbe husika kama haujasomeka, yaani ‘Mark as unread’

Kuanzia sasa utaweza kusoma na kisha kuufanya ujumbe kutoka kwa mtu flani kama vile bado haujafunguliwa. Lakini jambo ili haligeuzi mpangilio yaani muda wa ujumbe huo kufika. Wenyewe wanasema hii itakusaidia kama una mpango wa kumjibu mtu baadae. Ila kwa mtu mwingine kama ulikuwa umeruhusu muonesho wa alama ‘vema ya bluu’ (blue tick) kwa ujumbe uliosoma basi ata ukibadili ujumbe kuwa ‘unread’ kwa yule aliutuma hautabadilika, kwake utabakia kuonesha ya kwamba ushaosoma ujumbe huo.

2. Milio spesheli kwa watu mbalimbali

Utaweza kuweka milio ya kitofauti kwa mtu mmoja mmoja, ‘custom notifications’. Kwa mfano ungependa rafiki au ndugu flani akikupigia simu au kukutumia meseji kwa WhatsApp usikie wimbo/mlio flani wa kitofauti basi utaweza kufanya hivyo kuanzia sasa. Hii itawezeshwa hadi kwa masuala ya mtetemesho (vibration).

3. Nyamazisha miito kwa mtu mmoja mmoja (Mute)

Kwa muda mrefu uwezo wa kuzima mazungumzo ya kwenye makundi, yaani ‘Groups’ ulikuwa ushawezeshwa. Kuanzia sasa utaweza fanya hivyo hadi kwa namba moja moja. Kama usingependa kusikia mlio pale mtu flani akikutumia meseji pasi utaweza fanya hivyo kuanzia sasa. Utaweza kunyamazisha kwa muda wa masaa 8, wiki 1 au mwaka mmoja.

SOMA PIA  App 6 Bora Za Kamera Kwa Ajili Vifaa Vya Android!

4. Tumia kiasi kidogo cha Data Pale unapopiga simu za WhatsApp

Je uwezo wa kupiga na kupokea simu kupitia WhatsApp umekuwa unakula bando lako kwa kiasi kikubwa? Basi furahi kwa sasa, kwani utaweza kuchagua kama hautataka WhatsApp kutumia data kwa kiasi kikubwa kupitia mipangilia yake, ila fahamu jambo ili litakugharimu ubora/kiwango cha simu yako zinazopitia WhatsApp.Whatsapp3-1

SOMA PIA  Clubhouse, app yenye hatari ya kuathiri usikilizwaji wa mijadala redioni

Kuwezesha utumiaji mdogo wa data – Settings -> Chats and Calls’, shuka hadi eneo la chini kabisa utakuta chaguo jipya – “Low Data Usage”

5. Emoji mpya na chaguo la rangi zake

Emoji mpya mojawapo ni ya kidole cha kati

Emoji mpya mojawapo ni ya kidole cha kati

Pia utaweza kutumia Emoji kadhaa ambazo zilikuwa hazipatikani kabla, pia utaweza kuchagua aina ya rangi za emoji husika. Na katika hapa WhatsApp wameleta rasmi hadi Emoji ya kidole cha kati….. hatujasema uitumie Emoji hii ila jua tuu kwamba inapatikana..hahahhahahahaaaa

Je kipi kipya umekipenda zaidi? Tungependa kusikia kutoka kwako na endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya kiteknolojia.

Google Play -> WhatsApp

Comrade Mokiwa

Mbunifu na mpenda teknolojia.

Muanzilishi wa Teknokona, TechMsaada na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published.

TeknoKona Teknolojia Tanzania