Teknolojia inazidi kukua na katika ukuaji wake basi vitu vilivyokuwaga ni vikubwa vinazidi kuwa vidogo lakini wakati huo huo ndio vinaweza kufanya mambo mengi zaidi.
Kompyuta za miaka ya 1950 zilikuwa kwa kazi za kimahesabu zaidi na wala si kwa ajili ya kusikilizia muziki, kutazama filamu, ku’facebook 🙂 n.k.
Wakati siku hizi mtu mmoja anaweza akawa na kompyuta za aina mbalimbali kwa wakati mmoja – yaani simu ya mkononi, tableti, laptop, saa janja na vingine vingi kwa wakati mmoja wakati wa miaka ya 1950 iliitajika nguvu ya watu kadhaa kubeba kompyuta moja.
Tazama picha hii ya miaka ya 1950 huko nchini Marekani pale kompyuta mpya ilipokuwa inafikishwa kwa mnunuaji wake..kama hamjala ugali hamuifikishi kokote!
No Comment! Be the first one.