Embu fikiria! Jinsi ya kuangalia namba ya toleo la simu yako ya Android. Au kupata menu ya Lugha katika simu yako ya iPhone. Huwa inasumbua kiasi. Sasa fikiria kufanya hivyo kwa mtu asiyeona kabisa. Mwanzo ilikuwa haiwezekani kabisa, lakini sasa si kitu tena.
Shukrani ziwafikie magwiji wa simu janja ulimwenguni, kwa kuwezesha simu janja hizi ziweze kutumiwa hata na watu wenye matatizo ya kuona. Kwa kutumia sauti maalum zilizoundwa ndani ya simu, mtumiaji wa simu janja sasa anaweza kusomewa maandishi yanayoonekana katika kioo, kuchagua kilichopo, kutoka, kuandika ujumbe mfupi, barua pepe na kila kitu kinachoweza kufanyika katika simu janja.
Teknolojia ya utumiaji wa simu kupitia kuiambia au kuiuliza jambo au mambo inazidi kukua. Muda si mrefu haitaitaji wewe kuigusa simu yako, utazungumza nayo tuu na itafanya utakavyo

Mtumiaji wa simu janja, atawasha ishara mbalimbali katika simu yake, mfano kubonyeza mara moja kwa ajili ya kuperuzi na kutafuta vitufe vinavyopatikana katika kioo, na kubonyesha mara mbili kwa kuingia katika app au huduma hiyo.
“Ni suala la mtumiaji kujifunza na kuelewa baadhi ya matendo tu. Baada ya hapo ni mteremko.” Anaelezea mlemavu mmoja wa macho, na mtumiaji mkubwa wa simu janja. “Wakati iPhone walipokuja kwa mara ya kwanza mwaka 2007, tatizo la utumiaji wa teknolojia ya mguso (touch screen) lilikua kubwa kwa walemavu wa macho”
Lakini iPhone walitatua hilo mwaka 2009 kwa kuja na Sauti saidizi (VoiceOver) na kufanya mapinduzi kwa walemavu wa macho mwaka 2011 kwa kuzindua msaidizi binafsi, SIRI. SIRI, msaidizi muhimu na maarufu miongoni mwa watumiaji wa iPhone na iPad, amewezesha watu wenye matatizo ya macho, na hata wale wasio na matatizo ayo kutumia simu janja zao kwa urahisi zaidi, kama kuiamuru simu yako kupiga simu, kutuma barua pepe, kusoma ujumbe, ratiba za safari n.k.
SIRI inaweza pia kukujibu na kuzungumza nayo kama unazungumza na rafiki yako kwa karibu. Google wakazindua Talkback mwaka 2009, kisaidizi cha kusoma katika simu za Android na baadae msaidizi binafsi Google Now mwaka 2012. Simu za Microsoft zina vipengele vinavyofanana navyo kupitia teknolojia yao ya Cortana ambayo inapatikana pia katika Windows 10 kwenye kompyuta.

“Sasa naweza kutumia simu yangu sana, ata zaidi ya baadhi ya watu wanaoona vizuri.” Anasema Jennison Asuncion, kiongozi wa shirika la upatikanaji (Accessibility) moja nchini Marekani, ambaye pia ni kipofu.
Je ushawahi kutumia teknolojia hizi katika simu janja yako? Tuambie umeionaje? Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya kiteknolojia! Pia ungana nasi Twitter kupitia www.twitter.com/teknokona
No Comment! Be the first one.