Sawa ni kosa la kisheria kuendesha huku unatumia simu katika nchi nyingi lakini hii imewashangaza wengi, hata saa?. Hii imetokea huko Canada Mjini Toronto, polisi wamemsimamisha mwendesha gari (Jeffrey Macesin) na kumuandikia tiketi ya faini kwa kosa la kuendesha huku akitumia saa janja yake
Jamaa huyo, Jeffrey Macesin kutokea Pincourt alishangazwa na kitendo hicho na kusema kuwa hakujua kafanya kosa gani wakati polisi wanamsimamisha alipokuwa akiendesha. Alikuja kushangazwa baada ya kujua kuwa kosa lake lilikua ni kundesha huku akitumia saa janja yake.
Jeffrey alipata adhabu ya kulipa faini ya dola 120 za kikanada lakini alishangazwa sana na jambo hili. Madai yake alidhania kwamba anaruhusiwa kuangalia saa yake mpya (Apple watch) huku akiendesha gari yake kama atakuwa hatumii simu yake (Habofyi)
“Simu yangu ilikua kando wakati naichaji na pia nlichomeka waya katika redio na hii (saa) ndio niliyokuwa natumia kubadilishia miziki huku mikono yangu ikiwa katika usukani” — Jeffrey
Kifungu cha sheria kinachobana watumiaji wa vyombo ya moto katika barabara katika eneo tukio lilipotokea kinasema kuwa “No person may, while driving a road vehicle, use a handheld device that includes a telephone function.” yaani ikiwa na maana kuwa “Hakuna mtu yeyote anaruhusiwa (wakati anaendesha katika barabara ya vyombo vya moto) kutumia kifaa cha mkononi na hiyo inajumuisha simu” Sheria nyingine ziko hapa
Mwanasheria, Avi Levy, anaye jihusisha na kesi za usalama wa barabarani alisema kuwa ni mda tuu walitegemea kesi kama hiyo na hiyo haitakuwa ya mwisho
Jeffrey alijitetea sana na kusema kuwa yeye hakuwa anatumia simu yake, ni saa tuu na pia anafikiria kutafuta mwanasheria wa kumtetea mahakamani. Tuambie sehemu ya comment wewe unaonaje swala hili je ni sawa jamaa anastahili adhabu hii?
chanzo CTV
Mfumo huh ukija hapa kwetu Tanzania, ninadhani wengi wetu tutakuws hatuani. Kwani makosa ya kuendesha na kutumia vifaa vya mawasiliano ni makubwa.
Mwenda A. Bumbuli – Tanga.