fbpx
Google, Magari, Teknolojia

Huduma za Google kwenye Renault, Nissan na Mitsubishi

huduma-za-google-kwenye-renault-nissan-na-mitsubishi
Sambaza

Wakati unapoendesha gari unaweza ukahitaji usaidizi na kwa jinsi teknolojia ilivyoendelea vitu ambavyo unaweza ukavitumia kwenye Android/iOS kwa asilmia kubwa kwengye gari unaweza ukavipata, nazungumzia huduma za Google.

katika harakati za kuhangaika kuweza kufika mjini/sehemu nyimgine kwa wale wanaomiliki vyombo vya usafiri na wanapenda kukaribisha mambo ya teknolojia kwenye magari yao wanaweza wakafurahi wakisikia hii:

Magari Mitsubishi, Renault, Nissan yapo nchi nyingi za Afrika na iwapo unatumia moja ya gari hizo ni vyema ukafahamu kuwa Google wameamua kupeleka huduma za “Google Maps” na “Google Assistant“.

Huduma za Google
Google Assistant na Google Maps vimesogezwa kwenye Renault, Mitsubishi na Nissan.

Mpaka kufikia huduma hizo mbili kupatikana kwenye magari hayo ni hatua kubwa na pengine kilichosukuma ni mauzo yao ambapo mwaka 2017 kwa pamoja (Mitsubishi, Nissan na Renault) waliuza magari 10.6m duniani kote.

Programu endeshi ya Google, Android inatazamiwa kuwepo kwenye mamilioni ya magari duniani kote kuanzia mwaka 2021 na kuwezesha kufanya mambo kadha wa kadha.

Huduma za Google
Uwezekano wa programu endeshi ya Android kuwepo kwenye magari mpaka kufikia mwaka 2021.

Mambo yamebadilika na yanazidi kubadilika, Google wameona wanaweza kutanua wigo wa Android kutumika kwenye vitu mbalimbali.

Vyanzo: Reuters, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Apps za Android zaanza kutumika katika Laptop za Chrome OS
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|