fbpx

Android, apps, Google Photos, Teknolojia

Unafahamu kuwa Google Photos imeboreshwa?

unafahamu-kuwa-google-photos-imeboreshwa

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Ukuaji wa teknolojia ambao unaenda sambamba na utandawazi leo hii si ajabu kuona watu wamepunguza sana kuweka kumbukumbu za picha katika mtindo ambao unaweza kuzishika. Kwanini teknolojia imerahisisha vitu kwa kuja na vitu kama Google Photos, iCloud.

Na katika miaka ya karibuni ukinunua simu janja moja ya programu tumishi ambayo utaikuta ipo tayari kwenye rununu ni Google Photos. Lakini je, nini hasa kazi ya programu programu tumishi husika?

Kwa tafsiri isyo rasmi “Kitunza picha cha Google” ni programu tumishi ambayo inatunza picha, picha jongefu mahali ambapo mhusika (anayetumia kifaa cha Android) ataweza kupata vitu vyake hata mara baada ya kubadilisha simu janja/tabiti ya Android ilimradi tu arudishe barua pepe ileile aliyokuwa anaitumia kwenye kifaa chake cha zamani.

Google Photos
Google Photos inawezesha mtu kuweza kufikiavitu alivyovitunza huko bila ya hata kutumia intaneti.

Je, ni kitu gani ambacho kimeboreshwa kweye kitunza picha cha Google?

Watu ambao tumekuwa tukitumia mara kwa mara kitunza picha cha Google utakubaliana nami kuwa wakati tunataka kusambaza kitukutoka kwenye mfuko husika kwenda kwa mtu/watu au kikundi menyu yake ilikuwa unaisogeza kutokakulia kwenda kushoto lakini kwenye maboresho yaliyofanyika sasa unaweza kutengeneza kiunganishanishi au kubofya “More” kuweza kuona vipengele vyote kwa kwenda chini.

INAYOHUSIANA  Jiandae Kununua Kompyuta Zitakazokataa Matoleo ya Windows 7 na Windows 8.1
Google Photos
Mpangilio mpya wa vipengele vya kusambaza kitu kutoka kwenye kitunza picha cha Google.
Kushoto ni muonekano wa kitunza picha cha Google kabla ya kuboreshwa. Katikati na mwisho ni Google Photos iliyoboreshwa.

Mojaya sababu kwanini kuna picha zina karibu miaka kumi mpaka leo bado ninazo na uwezo wa kuziona muda wowote popote pale ni kwa sababu ya kutumia vyema kitunza picha cha Google. Ewe msomaji wetu unazungumziaje maboresho haya?

Chanzo: Android Police

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*