Wakati watumiaji wa toleo la Windows 7 na Windows 8 rasmi wataweza kupata toleo la Windows 10 kwa kulishusha na kupakua (download & upgrade) kutumia intaneti kwa wengine bado itabidi kununua toleo hili katika mfumo wa kawaida.
Imekuwa imezoeleka kwa miaka mingi Windows kuuzwa katika CD ila katika kipindi hiki inasemekana toleo la Windows 10 Home na Pro litauzika katika diski za USB. Inasemekana uamuzi huu utasaidia kwani kompyuta nyingi siku hizi zinatengenezwa bila eneo la CD na hivyo CD ni teknolojia inayoondoka taratibu.
Inasemekana USB flash diski moja itakuwa na matoleo yote ya Windows 10 Pro na Home, na USB Diski hiyo itauzika kwa si chini ya Tsh laki 3.
Microsoft bado hawajatangaza rasmi jinsi watakavyouza toleo la Windows 10 ila tayari taarifa kutoka kwenye baadhi maduka na mitandao inayouuza programu endeshaji inaonesha kutakuwa na diski za USB zenye matoleo hayo.
Toleo la Windows 10 linategemewa kuanza kupatikana rasmi tarehe 29 mwezi wa saba mwaka huu.
Endelea kusoma mtandao wako wa TeknoKona kuweza kupata habari zaidi. Je unadhani uamuzi huu ni sahihi?
No Comment! Be the first one.