Kuanzia leo watumiaji wapya wa Messenger hawatahitaji akaunti ya Facebook, badala yake watumiaji wapya wanaweza kutumia majina kamili na namba ya simu. Watumiaji wapya ambao watapenda kujiunga na messenger kwa kutumia akaunti zao za Facebook watakuwa na uhuru wa kufanya hivyo maana kutakuwa na kitufe kwa ajili ya kufanya hivyo lakini kwa wale ambao hawatataka kujiunga na Facebook basi watatumia majina na namba za simu.
Watumiaji wapya wataweza kuchagua kama wanataka kuunganisha akaunti yao ya Messenger kupitia namba zao za simu au kupitia akaunti za Facebook. Pia baada yakujiunga ata ikiwa ni kwa kutumia simu basi utaweza kuona orodha ya watumiaji wa app hiyo kama wewe ambao una namba zao katika simu yako. Kwa kifupi hii itakuwa kama vile WhatsaApp.
Facebook wamefanya haya mabadiliko ilikuongeza wigo kwa wafanyabiashara na makampuni yanayotumia mtandao huo yaweze kuwafikia wateja wengi zaidi hata wale ambao hawapo katika mtandao wa huo. Pamoja na mabadiliko hayo ila pia tumeshuhudia Facebook wakianzisha huduma ya malipo, magemu ya video huu ni ushahidi tosha kwamba wanataka kuhakikisha kwamba Messenger inakuwa na wateja wengi kushinda wapinzani wake.
Ingawa wakosoaji wake wanasema mabadiliko haya makubwa yaliyofanywa na Facebook yatasababisha huduma ya WhatsApp (ambayo pia inamilikiwa na Facebook) kupoteza umaarufu wake ulipo hivi sasa, lakini Facebook wamesema WhatsApp inawatumiaji wengi katika mabara ya Asia Amerika kusini na ulaya wakati Messanger ikiwa na watumiaji wengi huko Amerika ya kasikazini.
WhatsApp ina takribani watumiaji walio hai 800,000,000 hivi sasa wakati Messenger ina watumiaji walio hai takribani 600,000,000, kwa ujumla mitandao hii miwili inao watumiaji wapatao bilioni moja nukta nne ambayo ni sawa na asilimia 20 ya watu wote ulimwenguni.
Je unafurahia mabadiliko haya kutoka Facebook? Soma pia – Facebook Kuifanya Messenger Kuwa Zaidi Ya Messenger!
No Comment! Be the first one.