Pengine kifaa kingine ambacho Apple itawaletea wapenzi wa vifaa na huduma zake ni headphone, hapo kwa wale wapenda kutumia headphone kama katika kusikiliza miziki nakadhalika watakuwa wameguswa sana.
Kifaa hiki kitakuja katika rangi za kijivu, silva, bluu ya anga, kijani na pinki, naaaaaaam! machaguzi ni mengi kweli na hii ni kulingana na kila mtu anapenda rangi gani katika hizo ‘AirPods Max’ .

Apple wajisifia katika upande wa sauti, kwani wanadai kuwa kifaa chao kinatoa sauti na kuichuja vizuri, muundo mzuri na pia ina uwezo wa hali ya juu katika kuhakikisha kuwa inapunguza makelele.
kingine kizuri ni kwamba hawakuishia hapo, wameweka kipengele cha ‘Transparency mode’ hichi kitaweza kumfanya msikilizaji aweze kusikia mziki (kwa mfano) na mazingira yanayomzunguka kwa wakati mmoja.

Kwa karaka haraka fikiria ni kama AirPods tuu lakini hii inakua katika mfumo wa headphone. Chaji inakaa masaa 20, pia kama AirPods itakuwa inaruhusu matumizi ya Siri.
Kumbuka tangia kampuni ya Apple kuinunua kampuni ya Beats Electronics kwa zaidi ya dola za kimarekani bilioni tatu, kulikua na fununu nyingi sana kwamba kampuni hiyo itatengeneza Headphone…. wakati ndio umefika
Bidhaa hii itapatika kwa takribani dola za kimarekani $549 ambazo kwa haraka haraka ni sawa na shilingi 1,273,131/= za kitanzania.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika kisanduku cha maoni… kumbuka kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kwa daima tupo nawe katika teknolojia!
No Comment! Be the first one.