fbpx

Anga, Ndege, Teknolojia, Usafiri

Injini za Ndege kutoka Urusi: Ndege ya kwanza yaruka ikitumia Injini za Urusi

injini-za-ndege-kutoka-urusi-ndege-ya-kwanza-yaruka

Sambaza

Injini za ndege kutoka Urusi zilikuwa maarufu pia miaka mingi iliyopita kabla ya taifa hilo kuporomoka na kuvunjika kutoka Umoja wa Kisovyeti.  Baada ya miaka mingi sasa tayari ni rasmi utengenezaji wa injini za ndege kutoka kiwanda cha ndani cha taifa hilo umefanikiwa.

Jumanne ya wiki hii ndio kwa mara ya kwanza ndege iliruka nchini humo ikiwa inatumia injini zinazotengenezwa ndani ya nchi hiyo. Ndege hiyo inayokwenda kwa jina la MC-21, imetengenezwa na kampuni inayokwenda kwa jina la Irkut Corporation, injini zikitengenezwa na kampuni ya United Engine Coorporation  – asilimia kubwa ya umiliki katika makampuni hayo unamilikiwa na shirika la anga la Urusi la Rostec.

ndege ya mc 21 injini ya ndege kutoka urusi
Ndege ya MC 21

Majaribio ya ndege hiyo yalikuwa ya muda wa saa moja na dakika 25.

Serikali ya Urusi imekuwa imetaka kwa muda mrefu sekta hiyo irudi katika kiwango cha ubora wa juu ili kuweza kushindana na Boeing pamoja na Airbus – mashirika ya utengenezaji ndege ya Marekani na Ulaya.

Inategemewa wateja wa kwanza wa ndege ya MC-21 wataanza kupokea ndege zao kufikia mwisho wa mwaka huu. Hadi sasa kuna oda ndege 175 za MC-21, 50 kati yake zikiwa kutoka shirika la ndege la  kiserikali la Urusi, Aeroflot. Ndege hizi zinauwezo wa kubeba abiria 130 hadi 211.

SOMA PIA  Google Classroom yaboreshwa
ndege ya MC 21
Injini za Ndege kutoka Urusi: Ndege hii inaweza ikaleta ushindani kwa Airbus na Boeing katika eneo la ndege za masafa ya kati

Hii ni habari njema kwa makampuni ya ndege duniani kote kwani kwenye biashara ya ndege kwa sasa hakuna sana upinzani – soko limeshikiliwa zaidi na Airbus pamoja na Boeing. Tayari ata nchini China kuna shirika la utengenezaji ndege ambalo lipo kwenye hatua za majaribio. Wengi wanaamini ushindani huu utasaidia kushusha gharama za manunuzi ya ndege huko mbeleni.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Comrade Mokiwa

Comrade MokiwaMuanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COMMuda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.| mhariri@teknokona.com |

Toa Maoni

Your email address will not be published. Required fields are marked*