Watumiaji wa WhatsApp Web ni wengi tuu duniani kote wanaongezeka kila siku halikadhalika inazidi kuboreshwa kila mara ili kwenda na wakati lakini pia kuzudi kuongeza watu wanaoitumia.
Mimi ni mmoja kati ya wengi tuu ambao watumia WhatsApp Web katika mawasiliano yangu na nimekuwa nikishududia maboresho kila baada ya muda fulani. Uwezo wa kuhariri picha kwenye WhatsApp jambo hilo limekuwa likiwezekana kwenye Android/iOS tu lakini sasa mambo yanabadilika.
WhatsApp Web pamoja na ile ya kwenye kompyuta katika toleo jipya linawezesha watumiaji kuweza kuhariri picha (kama ilivyo kwenye WhatsApp ndani ya simu zetu) hivyo mtu kuweza kurekebisha picha kwa kuongeza nakshi nakshi au kupunguza kitu.
Kipengele hicho kipya (drawing tools) kinamuwezesha mtumiaji wa WhatsApp ya wavuti ama ile ya kwenye kompyuta kuweza kupunguza ukubwa wa picha (crop) kama vile ambavyo inaweza kufanyika kwenye simu janja kwa muda mrefu tuu kwa wale ambao wanatumia toleo la karibuni kabisa.

Maboresho yanayofanyika kwenye programu tumishi huwa yanaletwa ndani ya soko (App Store/Playstore) au kwa taarifa fupi inayoihusu programu tumishi husika. Kwa mantiki hiyo sasa ni lazima kuboresha programu tumishi kwa kushusha masasisho ili kuweza kuendana na mabadiliko yaliyofanyika.
Je, ewe msomaji wetu unayazungumziaje kipengele hicho kipya cha WhatsApp ya kwenye tovuti au ile ya kompyuta? Tupe maoni yako.
Vyanzo: Gadgets 360, mitandao mbalimbali
One Comment