Xiaomi imetangaza ujio wa saa janja (Smart Watch) kwa ajili ya watoto. Saa hizo zitajulikana kwa jina la Mi Bunny Watch 3 na zitakuwa na teknolojia ya 4G pamoja na sehemu ya kuwekea laini.
Pia saa hiyo itakuwa na uzito wa gramu 51, kioo chenye teknolojia ya AMOLED na kamera yenye 2MP HD. Aidha, itakuwa na rangi za aina mbili za Udhurungi na Bluu.
Ukubwa wa kioo chake utakuwa wa inchi 1.41 pamoja na teknolojia ya kulinda kioo hicho ya 2.5D Gorilla Glass. Pia kutakuwa na programu itakayosaidia kamera kutambua eneo ililopo kupitia kuwa na mawasiliano na GPS/A-GPS ambayo ipo ndani ya saa hiyo; hii inasaidia sana kumlinda mtoto aliyevaa saa hiyo kujua mahali alipo kama atapotea au kutekwa.
Betri ya saa hiyo ni nzuri na ina uwezo wa kukaa na chaji kwa muda wa saa 30 na kuchajiwa kwa muda wa dakika 50 tu.
Saa ya Xiaomi Mi Bunny kwa ajili ya watoto.
Kwa sasa saa hii inapatikana katika maduka mbalimbali nchini Uchina na kwenye maduka ya mtandaoni kwa kiasi kisichozidi Dola 90 za kimarekani ambapo ni karibia Tsh. 205,000/-.
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.